Mkuu Lagat...., swala la kuweka mizani kwenye barabara za changarawe ni la kawaida sana. Kumbuka kuwa pamoja na kwamba inaonekana kwamba barabara za changarawe ni za kawaida (non-engineered) ukweli ni kwamba nazo pia zinatakiwa kufanyiwa matengenezo ya kawaida na pia zinatakiwa ziwe na aina flani ya kuzuia magari yenye uzito zaidi ya kiwango kuzitumia kupunguza "premature failure". Tuelewe kwamba hata barabara za changarawe pia zimefanyiwa uhakiki (design) kwa kufuata viwango na kanuni za barabara za Tanzania kama nchi. Kuna nchi kama Sudan, Uganda, Namibia, Msumbiji ambapo wana barabara za changarawe na wanafanya udhibiti wa uzito pia. Kwa hili lazima tukubali ukweli kuwa lazima uzito udhibitiwe!!