Gerald .M Magembe
JF-Expert Member
- Jul 17, 2013
- 2,496
- 1,800
Sometimes nawaza kwamba kama CCM hawawezi kuweka fairness katika maswala ya siasa na chaguzi basi tuwe kama China na chama chao cha kicommunist.
Seems to me kwamba multiparty democracy zinahitaji watu waliokomaa kuvuka viwango vya ubinafsi, na nchi zetu hizi watawala hawawezi kuachia madaraka hivi hivi eti kwa sanduku la kura tu. Kwanza mfumo wa vyama vingi ni kama tulilazimishiwa tu.
Na hapo sijaenda kwenye hoja. Maana kama ningekuwa mshauri wa chama kikuu cha upinzani, ningewaambia kwamba baadhi ya hoja zenu nyingine ziko too radical kiasi cha kuwafanya watawala waliopo kufanya "kila linalowezekanika" kuhakikisha misingi ya nchi haivunjwi. Hata Jakaya (kiongozi aliyekuwa tayari walau kucompromise misingi na kuacommodate upinzani) wapinzani walipomfikisha eneo la kuyumbisha misingi mikuu ya nchi ikabidi astuke na kuwafukuzia mbali.
Sasa changanya ubinafsi na uroho wa madaraka + utawala wa CCM kuogopa misingi ya nchi kuvunjika chini utawala tofauti. If you can't fight'em join'em!
CCM inafuata rules za political contest za wachina.
1) ukikaribia wakati wa contest unatakiwa umchukie opponent wako kuliko sumu ya cynide.
2) Usimtafutie silaha ya kimo chake, tumia silaha ambayo ya mwisho na kubwa na yenye kufanya uharibifu kuliko silaha zote unazo zimiliki
3) Lazima ujitayarishe sana kama contest hiyo na usitoe nafasi yeyote ile ya kushindwa. Na ikitokea kashindwa basi uhai wake kisiasa upotee. Na kushindwa kwako ujue uhai wako kisiasa unapotea.
4) Mashambulizi yawe ya mazito sana ya muda mfupi with precision ambayo yatamuingia mwilini yote.
5) Katika contest hiyo kipigo hicho kiwe cha kummaliza na kummvuruga, na lazima kimuingie sawa sawa kiasi asijitambue.
Na ikitokea akapona basi lazima awe amechakaa sana hata achukue muda kuanza kupumua. Na hata akiweza kujikusanya lazima awe na hali mbaya kiasi akirudisha shambulizi liwe hafifu sana kiasi haliwezi kukudhuru.
6) Uhakikishe udhaifu uliomuingizia mwilini mwake uwe umenyong'onyea kwa maisha yake yote ya kisiasa na awe anaogopa political contest siku yeyote ile aambiwapo anapambana na wewe.