ITAKUSAIDIA HII; Tips za jikoni nyumbani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Ukimarinate nyama au samaki kwa viungo( vitunguu saum, tangawizi, masala) ongeza mafuta kidogo na mtindi vijiko viwili inalainika na kunoga

Ukikosa vanila unaweza saga Ganda la limao bichi kuleta harufu nzuri kwenye keki au chapati za maji

Ukitaka kupika mboga ya karanga, saga karanga kisha tumia maziwa kukorogea karanga badala ya maji inanoga sana

Chapat ukiógeza kdg nazi ya unga na ukakandia maziwa chapati inakuwa zaid ya nzuri

Ukitaka chips au ndiz ziwe nzuri, chemsha kdg dk 5 ipua zichuje maji then weka kwenye freezer.

Ukitaka kukaanga toa pasha mafuta choma usisubiri zitoke barafu, utastaajab radha yake

Ukiunguza wali penyeza mapande makubwa ya pilipili hoho ndani ya wali huwa inaondoa kabisa harufu ya kuungua

Ukiona mafuta yamekuwa mengi kwenye supu au mchuzi tumia mkate wa siles kupitisha juu kufyonza

Ukitaka maharage yawe na rojo zuri,baada ya kubandika tia mafuta ya kupikia yaivie pamoja

Ukitengeneza juice ya rosela au ubuyu unaweza weka mchaichai pale unapochemsha juice inavutia sana

Chapati ikilala ukitaka kuipasha iwe lain ichove kwenye maji baridi na kuitoa then pasha kwenye frypan bila mafuta..itakuwa kama umepika leo

Ukipika matembele ukiweka tangawiz na pilipili manga yanakuwa matamu balaa

Juice ya parachichi weka ndimu au limao utaipenda

Ukitaka samaki wabichi wasivurugike au kung'ang'ania wakati wa kukaanga. Wapake unga wa ngano wakolee halafu kaanga ni watamu mno

Ukitaka kubadili pishi la wali weka kitungú maji, saumu na iliki kdg wkt wa kuchemsha maji then yachuje halafu pika wali wako unanukia balaa

Kama unatumia gesi kupikia wali, jaribu tumia maji ya baridi kupikia mchele unanoga hasa

Ukitaka utumbo uive haraka weka limao pekee bila chumvi kwa yake maji ya kwanza.
 

Attachments

  • upload_2017-8-23_16-19-23.gif
    42 bytes · Views: 199
  • upload_2017-8-23_16-19-23.gif
    42 bytes · Views: 183
  • upload_2017-8-23_16-19-23.gif
    42 bytes · Views: 179
  • upload_2017-8-23_16-19-23.gif
    42 bytes · Views: 184
Kwenye wali mapande ya pilipili hoho unaikata kwanza au unaeka nzima? pia unaeza kueka kitunguu maji katikati ya sufuria kukata harufu ya kuungua.
 
Nimekuelewa mkuu kwenye wali na gesi sijakusoma ila Uzi mzur sana
 
Hapo kwenye gesi kupikia wali, maji ya baridi kivipi? fafanua.
 
Hapo kwenye gesi kupikia wali, maji ya baridi kivipi? fafanua.
Mchele ukishauosha, unauweka kwenye sufuria ya kupikia, kisha unatia maji yasiyochemchwa (baridi),chumvi na mafuta,koroga vizuri kisha bandika sufuria yako jikoni ikiwa imefunikwa vizuri!


Ni vizuri usigeuze wali mpaka maji yatakapokuwa yamekauka. Ila kumbuka kupunguza moto kwa kadri maji yanavyozidi kukauka
 
Asante sana
 
Tips nzuri sana, nita jaribu ya tembele tangawizi na pilipili manga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…