Itakuwa kesi ya karne spika wa bunge na wenzake mahakamani

Itakuwa kesi ya karne spika wa bunge na wenzake mahakamani

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Muhammad Ali bingwa wa masumbwi aliandika kitabu cha maisha yake, ‘’The Greatest My Own Story,’’ ambamo ndani yake ameeleza pigano lake na George Foreman kwa kirefu sana. Huyu George Foreman alipigananae mwaka wa 1974 na katika maisha yake yote katika masumbwi hapakutokea mpiganaji dhidi yake ambae watu waliona kuwa safari hii Ali atapigwa ila huyu Foreman.

Sababu kubwa ya watu na washabiki wa Ali kuona kuwa safari hii Ali hatovuka kiunzi ni kuwa Foreman alimpiga mpinzani mkubwa wa Ali, Joe Frazier katika raundi ya tatu na Frazier akiangushwa chini mara tatu katika raundi moja. Kila aliyepigana na Foreman alikuwa hakatizi raundi ya tatu anakuwa yuko chini hoi. Wengi wakadhani kuwa na Alii ataishia chini kama waliomtangulia kupigana na Foreman.

Katika hiki kitabu chake Ali aliweka sura akaipa jina, ‘’Bossman Comes,’’ katika sura hii ndimo alimoeleza pigano lake na Foreman kwa kirefu sana. Bossman ni jina la mpiganaji masumbwi wa uzito wa juu, pandikizi la jitu na alikuwa ndiyo, ‘’sparring partner, yaani mfanya mazoezi ya kupigana. Huyu Bosman ndiye Foreman akifanyanae mazoezi.

Ali katika mkakati wake wa mazoezi alitaka kujua kila kitu na mbinu zote za Foreman aliyekuwa na sifa za kuwamaliza wapinzani wake chini ya raundi ya tatu. Kwa ajili hii basi alimuajiri Bossman kama, ‘’sparring partner,’’ wake ili amfunze mbinu na kumpa siri za mpinzani wake Foreman ulingoni.

Ali alikuwa anafanya mazoezi ya raundi 30 kila siku akijitayarisha kwa pambano hilo.

Lakini Bossman alimuambia Ali bila kumficha kitu kuwa hatoweza kumpiga Foreman na akamueleza sababu zake kwa nini Ali atapigwa. Alimwambia Ali kuwa Foreman ana ngumi nzito na nguvu nyingi atakuwa anamsukuma nyuma kama karatasi. Ali alimuuliza Foreman, ‘’Niambie, Foreman anaweza kujitolea kufa ili ashinde abaki na taji?’’

Wakati ule Foreman ndiye alikuwa anashikilia taji la dunia la uzito wa juu.

Hapa Ali alitaka kujua ujasiri wa Foreman. Bossman alitingisha kichwa kuonyesha shaka. Katika pigano lile ilipofika raundi ya tatu Ali alikuwa bado yuko wima na akimrushia Foreman makonde ya uhakika.

Ali anasema alijua Foreman atachoka haraka na atampiga kwa sababu ngumi zake nyingi zilikuwa hazimpati zikiishia hewani na katika mchezo wa ngumi Ali anasema, hiyo ni dalili mbaya kwani mpiganaji anajichosha mwenyewe akimwacha mpinzani na nguvu zake.

Katika pigano lile Foreman alipigwa kwa, ‘’knockout.’’

Wataalamu wa masumbwi wanasema kilichomfanya Foreman apigwe ni kitu kimoja tu nacho ni kutegemea ushindi wa haraka wa raundi tatu. Foreman hakuwa amejitayarisha kwa safari ndefu ya jasho na damu. Ali alikuwa akifanya mazoezi ya raundi 30 ilhali masumbwi ni raundi 15.

Nimekileta kisa hiki cha Ali na Foreman kutaka kuwafikirisha wasomaji wangu. Nilikuwa nasoma hapa FB jinsi baadhi ya watu wanaomuunga mkono Prof. Lipumba walivyokuwa wamefurahishwa na kufukuzwa kwa wabunge 8 wa CUF na Spika wa Bunge kwa kasi ya ajabu kuwafuta ubunge na Tume ya Uchaguzi kupokea majina ya wabunge wapya walioteuliwa.

Lakini kilichonishangaza zaidi ni pale nilipoona katika TV jinsi baadhi ya hao "wabunge," walioteuliwa walivyokuwa wakijibu maswali na kufurahi na kuona kuwa tayari wameshakuwa washindi na weshaapiswa na kuwa wabunge. Nikawa najiuliza, ‘’Inakuwaje watu wetu wakawa na uwezo mdogo wa kutafakari mambo kiasi hiki kufikia kushindwa kuona kuwa hivi ni vita vikubwa na sasa vilikuwa vinaingia katika kipindi muhimu na kigumu kitakachoacha katika sakafu damu nyingi sana, inawezekanaje?’’

Ndipo kiliponijia hiki kisa cha Muhammad Ali na mipango yake ya kupigana pambano la muda mrefu na kwa mkakati huu akaibuka mshindi.

Mgogoro wa CUF sasa uko katika kipindi muhimu sana na Tanzania inaandika historia mpya. Wabunge 8 waliofukuzwa na Prof. Lipumba wamekwenda mahakamani na kwa mara ya kwanza Spika, Msajili wa Vyama Vya Siasa, Mkurugezi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na hao ‘’Wabunge,’’ waliochaguliwa na Prof. Lipumba watasimama mahakamani kujibu mashtaka kama washitakiwa. Haya si waliyotegemea hasa kwa hawa ‘’Wabunge,’’ watarajiwa, hawa hawakutegemea kabisa kushtakiwa.

Hivi sasa sakata hili linaingia katika safari ndefu ya nenda rudi, panda shuka ya mahakama. CUF wana uzoefu wa kutembea safari ndefu zenye shida, mihangaiko na damu na hii ndiyo silaha yao kubwa iliyowawezesha kuwapo hadi leo na kubaki wakiwa na nguvu kubwa juu ya shida zote walizopitia.

Kuanzia juzi naona hali imebadilika kwa upande waliokuwa wakifurahi kwa kupata ‘’Wabunge,’’ wapya. Ukweli wa hali halisi taratibu unazama na kueleweka uzito wake kuwa hii si safari ya raundi tatu alizotegemea Foreman bali hii sasa ni safari ya raundi 30 alizokuwa anazisubiri Ali na akawa amejitayarisha kwa safari ya mwendo mrefu. Ali alimuuliza Bossman ikiwa Foreman yuko tayari kufa kupata ushindi. Je, hawa wanaopelekwa makahamani bila ya khiyari zao wako tayari kubeba zigo hili zito ambalo hawakujitayarisha wala kutegemea?

Kwa kuhitimisha ningependa ieleweke kuwa pambano hili la Ali na Foreman la mwaka wa 1974 juu ya umaarufu wake si, ‘’Pambano la Karne,’’ kamwe. Pambano la Karne ni lile Ali alipopigana na Joe Frazier mwaka wa 1971 na Ali akashindwa kwa, ‘’points.’’

Ukifika Madison Square Garden, New York ambako ndipo walipopigana Ali na Frazier katika, ‘Pambano la Karne,’’ nje liko bango kubwa sana la wanamasumbwi hawa.

Naingia maktaba kutafuta picha ya bango hili nikiiipata nitaiweka hapa jamvini.

IIv2HetxsuRs8DlJLzAC1Iv0gkhvQC-hcwq9EGmJeTaO1_Or3YrJJquIANxtcQZLqgFzqawIeTm1tvLcCfdXMwPly0xHIo-EFHHmbKpsWfiyrQPY04F1nZS3LcRvrMJR5XdJ1GUsa9eY4aviX6RXnniq6jJUUzZeBXLlliuha7Wsggrq-CbebTemlTbDSxJfHl8nKMWWH8VAyjIzvkld0rHrKNjZaXJr_W0wP4GMACpMtMYXhX-YKhAF57UI28ajMEDS5VdWlHCtDb3M2aLD-e8qjyqh0AeZxAvS18AYewSDyq0-lgOj7jjhAw_jzN1Fy-jXZYxR0525r1dFMFW__zOkDJOWaxv9Rhbhr6Jrf3HQw-DGhI8FvClkQlhUDE67dq-XQsjj4rP--aUeJP2okbKx7B2Eji9SweCRfIL-z8spzRCQ46rAy67_Tq_LpUaU-eZslv3wp9j6TBqbPa2WygL0tiam6rpPad_W9wr-D5fnhwE_FAR99yNMMfnEGvu1kCF_v5F371HNmbUK18elcLKa1eIGb0E5Ps-3S-mUMc0nw3GUrQyuITVU9DNWjtypipHTdxBo_d7Zx4Jalc-kNSgJdWBFyq7QBLW2iV7ZZcbKLJGZMd8g=w406-h542-no
 
Mie mgonjwa na mpenzi wa ngumi hasa...Umenigusa!
Pambano unalolisema nimeliangalia zaidi ya mara tano kama yalivyo mapambano matatu ya Joe Freizer na Ali ..

Aidha ...
Mie mpenzi wa CUF na siasa za upande unaoonewa na ulio upande wa haki.

Kama kesi iko hivyo na itawahusisha hao nashukuru sana kwa taarifa hii.

Zaidi ya hapo nimekua na maumivu makali mno juu ya kinachoendelea.

Hata hivyo matokeo ya sasa ni yameletwa na gape nyingi sana zilizotengenezwa na akina Seif kwa kudhani Prof. ni mtu wa kawaida.
Kwa fikra zangu pale tu alipovamia mkutano wa Blue Pirl alitakiwa kufunguliwa kesi ya jinai haraka sana...kwani hakua mjumbe halali wa mkutano na wala hakualikwa.

Hiyo kesi ingelimtosha kumzuia kufanya mambo mengine yote anayoyafanya.

Asante kwa kututia moyo.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzi huu umeutafutia mfano "hai", lakini kwetu tusiofuatilia mambo ya kisiasa nchini, haujatushibisha na somo lako hili.
Umetuacha na maswali mengi kuliko majibu.
Umejenga maswali kutokana na kutodadavua kinagaubaga kuhusu mustakabali wa cuf badala yake umeegemea kushabikia mambo yaliyo katika sintofahamu.
Je mahakama imewekea pingamizi ya baraka alizopewa Lipumba na bunge kufukuza wabunge?
Je wabunge wateule wanashitakiwa kwa kosa gani?
Je spika wa bunge anashitakiwaje binafsi wakati bunge ni taasisi?
Je mahakama ya Tz, inamfahamu nani m/kiti halali wa cuf kati ya Seif na Lipumba?
Maswali kama haya ulitakiwa uyazibe kwa maelezo yaliyojitosheleza.
 
Nadhani watawala wetu baadhi wanadhani huu mpambano ni ule wa the rumble in the jungle lakini kwa mbali naona mantiki ya kuliita pambano la karne kutokana na viashiria fulani hivi

Anyway yangu macho
 
Kwa hiyo maalimu Seifu anajifunzia Chadema ili amuangushe Lipumba?

Ushauri wangu ni kwa maalimu kurudi buguruni na kumuomba msamaha lipumba...huwezi kutumia mamluki wa chadema kuihujumu cuf kwa manufaa yako...

Kubenea kamuumbua sana maalim
 
Nasubiri kwa hamu spika kupandishwa kizimbani.
 
Ivi siku lipumbavu alipotangaza ayo majina 8, ile spika si ilikua kwenye mkutano wa kugombea ubunge wa africa, alisain vp, au ndo mambo ya intaneti?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hili suala acheni wataalam wa sheria wazungumze. Mtizamo wa kisheria ni tofauti kabisa na mtizamo wa kisiasa kama wengi wanavyoona.
 
Sababu kubwa ya watu na washabiki wa Ali kuona kuwa safari hii Ali hatovuka kiunzi ni kuwa Foreman alimpiga mpinzani mkubwa wa Ali, Joe Frazier katika raundi ya tatu na Frazier akiangushwa chini mara tatu katika raundi moja. Kila aliyepigana na Foreman alikuwa hakatizi raundi ya tatu anakuwa yuko chini hoi. Wengi wakadhani kuwa na Alii ataishia chini kama waliomtangulia kupigana na Foreman.
Hii imenikumbusha Evandor Holy field alivyompindua al-haj Tyson.
 
Kaka Mohamed Said , Lipumba ni mtu wako wa karibu kiasi fulani, najua zile kampeni za mwazo za CUF wewe na Lipumba mlikuwa kwenye ukaribu wa aina gani

Hivi unaweza kutueleza ni nini kilichomfika Lipumba mpaka kufikia hatua ya kuwa kibaraka kiasi hichi?
 
WAKUU, UJUE HATA WALE WABUNGE WA VITI MAALUM WAPYA WALIOTEULIWA NA TUME, TUME HAIKUFUATA ORODHA YA MAJINA ILIYOWASILISHWA NA CUF! YANI NI MAJINA YAO BINAFSI.. MANA ORODHA INATAKIWA IFUATWE KULINGANA NA KURA AMBAZO WALIPGIWA KUTOKA WA JUU KWENDA CHINI..

HAPO NDO INAPOBIDI HATA HAO WALIOTEULIWA WASHTAKIWE KWA KUWA KIVYOVYOTE NA WAO WAMESHIRIK KWENYE HUO MCHEZO MCHAFU.
 
Kwa hiyo maalimu Seifu anajifunzia Chadema ili amuangushe Lipumba?

Ushauri wangu ni kwa maalimu kurudi buguruni na kumuomba msamaha lipumba...huwezi kutumia mamluki wa chadema kuihujumu cuf kwa manufaa yako...

Kubenea kamuumbua sana maalim
Kifupi ni kuwa ID yako inakufaa sana
 
WAKUU, UJUE HATA WALE WABUNGE WA VITI MAALUM WAPYA WALIOTEULIWA NA TUME, TUME HAIKUFUATA ORODHA YA MAJINA ILIYOWASILISHWA NA CUF! YANI NI MAJINA YAO BINAFSI.. MANA ORODHA INATAKIWA IFUATWE KULINGANA NA KURA AMBAZO WALIPGIWA KUTOKA WA JUU KWENDA CHINI..

HAPO NDO INAPOBIDI HATA HAO WALIOTEULIWA WASHTAKIWE KWA KUWA KIVYOVYOTE NA WAO WAMESHIRIK KWENYE HUO MCHEZO MCHAFU.
Sidhan kama CUF walipiga kura kuchagua Wabunge Viti Maalum,waliandika tu viongozi.
 
Back
Top Bottom