Italia: Wadukuzi wadai kuiba GB 60 za taarifa za watu

Italia: Wadukuzi wadai kuiba GB 60 za taarifa za watu

Sam Gidori

Senior Member
Joined
Sep 7, 2020
Posts
165
Reaction score
417
Shirika la Usalama wa Taarifa za Mtandaoni nchini Italia linachunguza jinsi wadukuzi walivyofanikiwa kuiba taarifa za wafanyakazi na watumiaji waliosajiliwa wa Shirika la Hakimiliki la Taifa.

Kundi hilo la Wadukuzi linalojiita ‘Everest’ limedai kuwa linamiliki zaidi ya Gigabaiti 60 za taarifa walizoiba, ikiwa ni pamoja na Vitambulisho vya Taifa, Leseni za Udereva na taarifa zingine, baadhi zikiwa za watu maarufu nchini humo.


Wadukuzi hao wanataka malipo ya dola 500,000 za Marekani (sawa na Tsh. milioni 152.5) baada ya takwa la awali kutofikiwa.


Shambulizi hili dhidi ya Taasisi ya Serikali linakuja wiki chache tu baada wadukuzi nchini Argentina kufanikiwa kudukua taarifa za raia wote wa nchi hiyo kutoka katika Kanzidata ya Taifa na kuzichapisha mtandaoni, ikiwamo taarifa za Rais wa Taifa hilo, waandishi wa habari na mchezaji Lionel Messi.


Chanzo: RT

1634982003872.png
 
Msiwape hata mia. Mkiwadekeza kila siku watakuwa wanawatoa upepo.
 
Wekeni ulinzi wakati mnaongea nao wakirudi wakute Ukuta.
 
natamani sana kua hacker mkubwa kama kuna mtu anaweza akanipa muongozo tafadhali nipe maelekezo ...
 
Back
Top Bottom