Itel S11 Inatisha!!!! (Sitanii naombeni "LIKES" zenu nishinde itel S11 shindano la insha))

Wolle Melkas Fernando

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2016
Posts
253
Reaction score
360
1. CAMERA:

Simu hii ina Camera bora zaidi ambayo inafaa sana kwa selfie (kupigia picha kwa camera ya mbele/kuselfika)

Upekee wa camera hii ni kwamba ina upana mkubwa kuchukua eneo kubwa la picha yako (yaani ni wide angle 84°), hii inamaanisha unaweza kupiga selfie ya watu zaidi ya 10 na wote mkaonekana kwenye screen.
Camera hii ya itel S11 ina kitu kinaitwa face beauty mode ambapo, ukitumia hii mode inawezesha picha yako kuwa na uangavu mzuri na mvuto wa hali ya juu.


Zaidi ya hayo, simu hii ina LED flash mbili (dual led flash) ambazo huwezesha mwanga wa kutosha kuchukuwa picha nzuri hata sehemu yenye giza au yenye mwanga hafifu, picha inatoka nzuri na ubora uleule kama mchana, haijalishi usiku au mchana ni mwendo wa Ku-snap tu ukiwa na itel S11.

Camera ya itel S11 imeundwa kwa ‘Panorama mode’ ambayo huwezesha picha yako kuchukuliwa kwa upana unaoutaka na kuleta uhalisia wa mazingira ya picha uliyopiga (Enables to Cover original and wide landscape



Simu ya itel S11 screen yake imeundwa kwa teknolojia ya IPS ambayo ni ‘super bright’ hii siyo screen ya kawaida. Screen hii inafanya picha yako kung’aa na kuwa na mvuto zaidi.


1. SIFA NYINGINEZO:
Kwa upande mwingine Itel S11 ina ROM GB 8, hii inakusaidia kuhifadhi mafaili na vitu vyako vingi zikiwemo picha, huna haja ya kufuta mafaili yako. Pia kama utahitaji memory card basi unaweza kuweka memory card mpaka yenye GB 32. Itel S11 ina RAM GB1 ambayo inasaidia kuendesha mifumo ya simu yako kwa haraka na wepesi zaidi, hii inasaidia simu yako kutokuwa nzito.

Simu hii ya itel S11 ni nyembamba sana na inabebeka kirahisi (portable) ina wembamba wa 8.7mm (milimita) sawa na vipande 35 vya karatasi za rim vilivyopangana kimojakimoja, umbo la itel S11 linakufanya uone fahari wakati wote ikiwa kiganjani mwako.

Itel S11 ina teknolojia yaku-freeze mafaili yako, ambapo kama kuna mafaili ambayo hutumii kwa wakati huo na hutaki yabane nafasi kwenye simu yako lakini wakati huohuo unaona kuna umuhimu wa kuyatumia baadaye basi huna haja ya kufuta, utakachotakiwa kufanya ni ku-freeze tu mafaili yako. Uki-freeze hayatabana nafasi na yatakuwa kama vile hayapo lakini siku ukihitaji una-Unfreeze tu kisha yanatokea na bado hayatachukua nafasi kwenye simu yako tena (Hayatamaliza nafasi, yataendelea kuwa kwenye hali yaku-freeze ingawa unayaona na kutumia. Ukiwa na simu ya itel S11 huna hofu ya kufuta vitu vyako.

2. HUDUMA BAADA YA MAUZO (After sales service)

Ukinunua itel S11 huna haja ya kuwa na hofu kwani ina warantii ya mwaka mzima, na unaweza kupata huduma zetu kwenye vituo vyetu vya huduma kwa wateja (CarlCare) vilivyoko nchini kote.

Itel S11 sasa inapatikana nchi nzima kwa bei rahisi sana.
Taarifa zaidi bofya hapa: itel Mobile | Facebook

 
Ukinunua simu ya Itel jua kabisa kwamba imekula kwako.
 
Camera imeboreshwa ina MP5 lakini imewekewa kitu kinaitwa face beauty mode ambacho kinasaidia kufanya picha kuwa yenye ubora zaidi ya MP8. We tupia like, mi nishinde jamaaa,,,
Hapan kwasababu sio simu nzur acha kuipamba mkuu
 
Hivi hii kampuni haikufa wakati wa vita ya Kagera!!!

Kuna kampuni zina roho ngumu sana
 
UNATAKA KUTRACK INFO ZA WATU...
Ikumbukwe kua uklike page ya mtu FB unakuwa umetuma friend request .....hii itamrahisishia kufahamu info za mtu ...KUWENI MAKINI. .
 
Camera imeboreshwa ina MP5 lakini imewekewa kitu kinaitwa face beauty mode ambacho kinasaidia kufanya picha kuwa yenye ubora zaidi ya MP8. We tupia like, mi nishinde jamaaa,,,
bado mbayaaaa hat sio simu iyooo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…