SoC03 Ithibati ya katika Tasnia ya Uandishi Vitabu Tanzania

SoC03 Ithibati ya katika Tasnia ya Uandishi Vitabu Tanzania

Stories of Change - 2023 Competition

Alfris

Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
6
Reaction score
9
MAANA YA KICHWA CHA HABARI
Natumia neno Ithibati nikiwa na maana ya Kibali cha uchapaji wa kitabu. Tunaweza kuwa pia na neno "Uthibitisho", ambapo kwa Kilatini kuna neno "Imprimatur". (Rejea MobiTuki).

SABABU ZA KUANDIKA
Sababu ya kuandika haya, ni uwepo wa vitabu vingi kwenye mzunguko wa wasomaji, vyenye haki miliki, vyenye namba ya uthibitisho wa kimataifa (ISBN), na vinauzwa na kusomwa, lakini havikidhi vigezo vya ki-uandishi.

IDARA HUSIKA
Tanzania tuna Idara inayohusika na kutoa namba za umiliki na uthibitisho wa vigezo vya kimataifa "ISBN", ambao ni MAKTABA KUU YA TAIFA.

MAMBO YALIVYO KI-MAZOEA
Kwa sasa, yapo mazoea kwamba, mhitaji akiomba kupata namba hiyo, akiwaonesha tu Kichwa cha habari, badi hata kama hajachapa kazi, ama hata kama kazi haina viwango, akishalipia tu gharama husika, atapewa hiyo ISBN.

MADHARA YAKE
Kwa sasa, kuna mzunguko mkubwa wa vitabu vyenye makosa makubwa ya kiuandishi, makosa ya kisarufi na kifasihi kwa upande wa kiswahili, makosa ya kunakili bila rejea (plagiarism), makosa ya kutafsiri bila kutambua mwandhishi wa kwanza, na hata makosa ya kulisha wasomaji taarifa za uwongo, hada pale mchapaji anapoongea mada ambayo yeye siyo mbobezi, ila mchochezi.

Madhara yake ni pamoja na kuharibu lugha, kuondoa hadhi ya tasnia, na kuuwa ari ya utafiti.

MAPENDEKEZO
1.Mwandishi asipewe ISBN bila ya kuonesha uthibitisho wa kazi yake kwa njia ya maandishi, kutoka kwa mamlaka ama kiongozi mwenye taaluma inayotosha kuthibitisha makala yake.
2. Pia, apeleke copy ya kazi yake kwa Idara husika, ili waridhie kuwa ina vigezo vya kimataifa.
3. Maandishi yanayochochea ugomvi wa ki itikadi, yapimwe kwa hoja na nia. Kama yanalenga kusahihisha, yakubalike. Kama lengo ni kuonesha mapungufu bila kutoa suluhisho, yapuuzwe.

SULUHISHO
1. Vigezo vya uandhishi kwa ngazi za vyuo vyote, vifundishwe vema (methodology).
2. Wakufunzi wawe makini sana kusahihisha kazi za kibuandishi bila kupendelea.
3. Uaminifu kwa lugha ya uandishi uzingatiwe


REJEA
Nimeambatanisha sehemu ya Kava la kitabu cha mwandishi wa ki-Tanzania,. Nimefifisha jina lake na kuficha utambulisho wowote.
Katika makosa kwenye kava, utaona maneno kijij, badala ya Kijiji, ktk/katik- badala ya Katika; shule y, elimu y,; na pia ameandika aya zote kwa herufi kubwa. Na kitabu kimepewa ISBN Namba.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom