ITIKAFU ni nini?

Status
Not open for further replies.

nyiondo

Senior Member
Joined
Jan 14, 2013
Posts
149
Reaction score
24
Watanzania,
Naomba kufahamishwa 'itikafu' maana yake ni nini?
Lengo lake ni nini?
Nimeshangazwa na habari hii ya kusikitisha kutoka gazeti la mwananchi la leo.
Kama kiongozi wa nchi anasomewa itikafu ili 'AFE' je kajamba nani watasalimika vipi?
Lakini Mungu wetu ni mwenye nguvu sana. Mungu atakulinda Rais wetu.
 
Itikafu ni maombi maalumu yanayofanywa na kundi la waumini wa dini ili kumshitaki mtu kwa M/mungu kwa kuwaonea!!
 
Itikafu=ITIQAF.Neno hilo ni lakabu ya kiarabu. Itiqaf, ni ile hali ukaayo mahsusi kumuomba na kumlilia Mwenyezi Mungu juu ya yote yanayokusibu au kuomba msaada. Mara nyingi Itiqaf hufanyika katika zile siku 10 za mwisho wa mfungo wa mwezi wa Ramadhani. Ambapo wachamungu wa kweli hukaa misikitini pasipo kujihusisha na masuala mengine yeyote ya kimaisha au kidunia wala kuongea na waaminio waingiao kusali zaidi ya 'Assalaam alaikhum' pekee. Kwamba waaminio wanaokaa Itiqaf basi muda wao wooote wa hizo siku 10 hutumika katika ibada tu, yaani kuongea na Mwenyezi Mungu tu. Mwisho huwa ni mwezi unapoandama na kuthibitishwa kuwa siku inayofuata ni Eid.JK amechanganya mambo, kuna kitu huitwa 'MUBAHALA'. Mubahala ndio hutumika rasmi kuamua NGUVU ya Muumba ichukue hatua. Tena Mubahala huwa ni wazi ambapo mshitaki na mshitakiwa wote hupeana taarifa rasmi (kubainisha muongo na mkweli), (apokelewaye dua na asiyepokelewa dua). Mubahala hutoa idadi ya siku maalum hukumu ya Muumba kuwa imetolewa.JK kachanganya kati ya 'itiqaf' na 'mubahala', anapaswa aingiliapo masuala ya dini awahusishe wanazuoni wa kiislam kumpatia tafsiri yenye tafsida nzuri kwa umma.Rock City.
 
Labda kuongezea kwa mleta mada, iliwahi kuwa effective? Kuna mtu/watu waliwahi kufa/kudhurika kwa hii kitu, nina wasiwasi maana raisi juzi alilitamka hili huku akicheka.
 
Labda kuongezea kwa mleta mada, iliwahi kuwa effective? Kuna mtu/watu waliwahi kufa/kudhurika kwa hii kitu, nina wasiwasi maana raisi juzi alilitamka hili huku akicheka.
M/mungu huwa haipokei dua hiyo endapo mtu anayesomewa/ombewa yupo kwenye haki ya upendo wa watu wote anaowatawala bila kujali dini zao.
 

Kwa kuongezea hii inaonekana kuwapata masini tu....kwani waarabu walisha waombea sana maraisi wa Marekani wafe, au washindwe vita huko iraq, afghanistan n.k.......lakini haisadii kabisa waarabu wanapigwa viba na kushindwa vita vibaya.. huku maraisi wa marekani wakiendelea kuishi maisha yao kwa afya njema.
 
Damu ya Yesu itamlinda rais wetu Jakaya Mrisho Kikwete dhidi ya nia ovu ya kishetani inayotaka kumdhuru afe, vyovyote vile inavyoitwa, aidha itikafu au mubahala

Umeshasahau ulinzi wa nguvu usioonekana wa shekh YAHAYA (R.I.P.) unaomlinda? Damu ya Yesu na ulinzi wa nguvu usioonekana husemekana havichangamani!
 

Mbona ajafa sasa, kwa maana hiyo we dont need to worry what such nonsensical ritual entails, huyu Mr.President na hizi irrational thinking zake wakati mwengine, no wonder ghorofa lina anguka we unasema kazi ya mungu how about uzembe?

By the way muhusika huko angani kama unapita kuchunguliaga JF im only joking, we una nguvu lakini si hawa masheikh uchwara wanaotaka kukufanyia kazi yako ya kuchukua roho ya mwanadamu, ajabu yenyewe Mr President kaogopa ama nayeye mshirikina.
 
Itikafu ni maombi maalumu yanayofanywa na kundi la waumini wa dini ili kumshitaki mtu kwa M/mungu kwa kuwaonea!!

Itikafu ni "kujifunga" ....kilugha

Ama kisheria, itikafu ni kujifunga katika sala na ibada nyengine katika kumuomba Muumba

Ombi hilo linaweza kuomba ubarikiwe afya, mji upate mvua, na mengineyo
 
Ni sehemu gani katika bara Arab waarabu waliwaombea marais wa Marekani wafe?

Lakushindwa vita Iraq na Afghanistan ni kweli na umejionea mwenyewe jinsi Marekani anavyoshindwa Afghanistan na Iraq kijeshi, kimorali na KIUCHUMI.
 
Huyu ------ sijui kweli ni Muislam au kanyaboya tu!! Kuna uhusiano gani kati ya ITIQAF na kuombewa adhabu kwa Mungu? Alikuwa anamaanisha AL BADR au nini? ITIQAF ni ibada inayofanyika kwenye kumi la mwisho la mwezi wa Ramadhan kuomba maghafillah(msamaha na kumtaka Mungu akunyooshee mahitaji yako), sasa inauhusiano gani na yeye kuombewa afe?

Kumbe jamaa ni dhaifu hadi kwenye dini yake duh!Kweli ni janga la dunia!!
 
Ni sehemu gani katika bara Arab waarabu waliwaombea marais wa Marekani wafe?

Lakushindwa vita Iraq na Afghanistan ni kweli na umejionea mwenyewe jinsi Marekani anavyoshindwa Afghanistan na Iraq kijeshi, kimorali na KIUCHUMI.
Yeah, Marekani ameshindwa vita licha ya kumkamata Saddam akiwa hai, kumkamata Osama akiwa hai, kuendelea kuwa na majeshi ndani ya Iraq na Afghanistan na kusababisha mvurugano baina ya wananchi ndani ya nchi husika. Iraq na Afghanistan zilishinda vita, licha ya kuwa Marekani bado ina vikosi kwenye ardhi zao!
 
Labda kuongezea kwa mleta mada, iliwahi kuwa effective? Kuna mtu/watu waliwahi kufa/kudhurika kwa hii kitu, nina wasiwasi maana raisi juzi alilitamka hili huku akicheka.
1994 baada ya kadhia ya Mabucha ya Nguruwe Mrema alisomewa juilize alipo, Ali Ameir Mohamed alisomewa baada ya Mauaji ya Mwembechai hivi sasa yupo kama hayupo, Askof Lwambano baada ya kusomewa kafumaniwa kafukuzwa Kanisani Mburahati, Chenge baada ya kupitisha sheria ya Ugaidi akasomewa muda mfupi baadae likafumuka la vijisent akaporomoka kutoka kwenye uwaziri, Sofia kawawa kwa watu wazima wanaijua kadhia ya 1988 habari yake muulize Vita kawawa, hii kitu ni maombi ya kumshtakia Mwnz mungu kama huna hatia hakuna neno ila kama kwenye Dhulma ya Waislam wakapatikana kweli wachamungu lazima upate khabar yake, Kama jakaya anadhulumu waislam kweli ajiandae!
 

unachanganya mambo mzee,hutakiwi kuwa professional wa dini husika ili uiamini!
 
ungejua kuwa Uislam na uarabu ni vitu tofauti usingeandika ulichoandika, Hujui kuwa hata makanisa ya ufufuo Misri yanachimbua majini kwa lugha ya kiarabu
 

huu ni upepo tu, utapita.
 
unachanganya mambo mzee,hutakiwi kuwa professional wa dini husika ili uiamini!


Mbona sikuelewi mkuu? Kwa muumini wa kawaida tu wa kiislamu wala asiye ulamaa mwenye elimu kubwa ya kidini, hawezi kushindwa kutofautisha ITIQAF na AL BADR . Wewe nauhakika siyo muislam ndiyo maana unanishangaa nikimuita huyo mtu ni dhaifu kwenye dini yake. Tafuta mtoto mdogo wa kiislamu akuambie nini maana ya itiqaf halafu utafuta corelation na matumizi yake kwenye hotuba ya rais wako uone udhaifu wake.
 
Yeah, Marekani ameshindwa vita licha ya kumkamata Saddam akiwa hai,
Kama unafikiri kuwa waliteketeza mabilioni ya mapesa yao kwa ajili ya kumkamata Saddam hai basi jijue kuwa una tatizo!
Walikuwa na nafasi ya kumkamata Saddam hai katika vita ya gulf ya kwanza pale alipoivamia Kuwait...hawakufanya hivyo!
Jabulani said:
Iraq na Afghanistan zilishinda vita, licha ya kuwa Marekani bado ina vikosi kwenye ardhi zao!
Marekani hakuwa na haja ya kupoteza mabilioni ya pesa zake kwa ajili ya kuweka vikosi vyake Iraq na Afghanistani.
Kumbuka wana sehemu kubwa ya vikosi vyao Kuwait, Qatar na saudi Arabia!
Unafikiri ni kwa nini Marekani aliivamia Iraq na vipi alitimiza malengo yake?
 
Wange washirikisha watanzania wote tukafinga kwa siku kumi tu pengine tungeshafanya uchaguzi..kuna yule jaji alieshirikianana ikulu kumpoka ubunge lema hajafatu maana watu walifunga kwa siku saba nikasikia kakimbizwa india
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…