ITV dk 45: Rais Karume akiri kuandaliwa kuwa Rais wa Zanzibar

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
6,547
Reaction score
7,167
Rais wa zanzibar 2000 hadi 2010 Amani Abeid Karume, akiri kuandaliwa kuchukua wadhifa huo.

Akihojiwa ktk kipindi cha ITV DK 45 leo usiku, amesema aliitwa na wazee na kuambiwa Dkt Salmin anamaliza muda wake "Tunataka wewe uwe Rais"

Baada ya hapo alienda kuchukua fomu ya urais na ktk mchujo alishinda yeye.

SWALI: Kumbe mgombea urais huandaliwa mapema na wale wagombea wengine ni wasindikizaji tu? Je, wagombea wengine huwa wanajua juu ya mmoja wao kuandaliwa?
 
SWALI: Kumbe mgombea urais huandaliwa mapema na wale wagombea wengine ni wasindikizaji tu?
2015 Membe, January na Lowasa waliandaliwa. Bahati mbaya mtifuano ulivyotokea akapewa ambaye hakuandaliwa.

Matokeo yake alichokifanya huyu ambaye hakuandaliwa ni aibu kwa taifa. Aliifunga nchi ikawa kisiwa,aliwagawa watanzania kwa misingi ya kikanda, kisiasa na kikabila.

Kaja huyu naye ambaye kachukua kwa kudra za Mungu, nchi kaiweka autopilot.
 
Hatari
 
Makamu Mwenyekiti wa Chadema anaandaliwa kua mgombea Urais wa NCCR-Mageuzi πŸ’

Lakini pia mkurugenzi mtendaji wa jukwaa la Sauti ya waTanzania anaandaliwa kua mgombea Urais wa Chadema πŸ’

kwahiyo vyama vya siasa vinajitahidi sana kwenye maandalizi ya uongozi. Na wanakwenda vizuri πŸ’
 
Wewe unafikiri ati vijikaratasi vinavyoingia kwenye boksi vina saidia?
 
Nadhani ni jambo la kichama zaidi...wanaangaliana nani wa kumuachia kijiti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…