Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Ukiwa ni mfuatiliaji wa series fulani kwenye TV fulani au tamthilia mbalimbali, Series hizo na tamthilia hizo zina urahibu fulani, hivyo wakati wa tamthilia hiyo ukifika, wapenzi wa tamthilia hizo, huacha kila kitu ili kufuatilia tamthilia hizo.
Sasa kunapotokea matukio ya kitaifa au shughuli za matukio ya Mhe. Rais, yanayotangazwa live mubashara na TBC, ITV mnapoamua kujiunga, au wenyewe kutangaza mubashara, kwanza hili ni jambo jema, huu ni uzalendo wa ITV kwa taifa letu, hivyo natoa pongezi kwa ITV kwa uzalendo huu.
Pili nawaomba mtutendee haki sisi watazamaji wenu, na haswa waraibu wa tamthilia zenu ikiwemo Isidingo, mnapokatisha tamthilia kwa ajili ya matangazo mubashara, then tafuteni muda mwingine, mfidie kuturushia tamthilia mlizo zikatiza ili msitutese sisi waraibu wa tamthilia zenu.
Mfano hai ni leo. Mimi ni mpenzi wa tamthilia ya Isidingo ambayo marudio ya wiki nzima huonyeshwa siku za Jumapili kuanzia saa 4:00 asabuhi. Lakini leo, kutokana na tukio muhimu la rais Magufuli ikulu ya Chamwino Dodoma, ITV imekatisha marudio ya Isidingo na kutuletea matangazo ya mubashara ya Dodoma.
Hivyo tunaomba mtafute muda kuifidia Isidingo mliyotukatisha, mtanisamehe bure, uraibu ni uraibu tuu, ukikatishwa ghafla, kitu ambacho una uraibu nacho, kwanza unakasirika, pili unataka kuzima TV kwa hasira, ndipo unagundua hilo tukio ni muhimu sana kuliko tamthilia, hivyo unajikuta unaendelea kuangalia.
A Way Forward ili Tusikwazane.
Kwa vile ITV mna king'amuzi chenu, wekeni a dedicated channel ya tamthilia, na kuwa na PVR kama ilivyo DSTV Explora, ukisha set record the entire episodes, then PVR inakurekodia halafu wewe utaangalia kwa wakati wako, hivyo ITV mnakuwa huru hata kutangaza live za kila kitu bila kuwakera watazamaji.
Nawatakia mubashara njema
Na Jumapili Njema.
Paskali