ITV kipima joto leo wana agenda ya siri!

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Leo hii katika kipindi cha ITV cha malumbano ya hoja,wanajadili hoja inayouliza, mfumo wa muungano wa serikali tatu.Je,ni kuimarisha au kuudhoofisha muungano?

Cha kushangaza, karibu asilimia 99 ya wanaoshiriki wanapinga vikali muundo wa serikali 3 na kumshambulia mzee Warioba na tume yake vikali mno!

MY TAKE:
Hawa watu bila shaka wamekusanywa kwa agenda moja tu ya kutetea serikali mbili.

ITV wajitafakari sana.
 
Huyo jamaa wa tume anawakalisha sana, huyo dr. Wa bagamoyo ni type ya kina mrema lyatonga
 
:A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up: PAMOJA KAKA
 
Pro-Chadema kila kukicha na malalamiko leo tena ITV wamekuwa wabaya.
 
ITV nilikuwa na nawaheshimu sana ila leo mmekubali kununuliwa na magamba kuwasaliti wananchi,98% ya washiriki wa leo ni zile type za wanywa kahawa tu
 
Ni kamishana wa tume tu ndie alietetea mapendekezo ya tume ila wengine wote wako against na serikali 3.

Kuanzia leo sitakuwa na imani na hiki kipindi.
 
Nilikuwa nadhani Kibamba ni pro Chadema kumbe ni Non Aligned Citzen anayesimamia ukweli wa jambo amenifurahisha sana
 

itv wana ajenda ya siri nyuma ya mada ihi,watu wote ni ccm na michango yao nadhani umeisikia ni pumba tupu,leo nimemdharau bw kibamba nae ni mnafiki mkubwa huyu,
 

Nimeipenda ile ya kamshina wa tume "watanzania msiogope hata TFF ina raisi"
 
Nilikuwa nadhani Kibamba ni pro Chadema kumbe ni Non Aligned Citzen anayesimamia ukweli wa jambo amenifurahisha sana

Nani angejua zzk wa kabla ya 2008 angekuja kuwa msaliti?! muda utamuhukumu kwa kutaja kundi alilopo hata huyu unayemtaja!
 
Leo nimeshangaa wachangiaji walikuwa wachache tofauti na siku zingine, mfano mimi leo sijaona mwanamke humo ndani
 
Ni kamishana wa tume tu ndie alietetea mapendekezo ya tume ila wengine wote wako against na serikali 3.

Kuanzia leo sitakuwa na imani na hiki kipindi.

Ninaamini kwa asilimia kubwa kampeni zimeanza kati ya wanaotaka serekali TATU au MBILI ingawa si rasmi
 
Kibamba tangu apigwe biti na Jk amekuwa akitumia sehemu ndogo sana ya ubongo wake anapojadili mambo yenye kugusa maslahi ya ccm na dola!Amekuwa akiongea kwa msisitizo vitu ambavyo haviamini na hata uso unaonyesha.Kuvaa umbumbumbu wakati ulishauacha ni jambo gumu sana lakini huyu mwenzetu anajaribu sana kuuvaa sijui anataka kuteuliwa kwenye bunge la katiba?Yaani unamlaumu Warioba eti alihoji watanazania milioni moja tu na unauliza eti milioni 44 wako wapi?!!!Yaani leo Kibamba hujui kuwa kuna watoto wengi kati ya kundi hilo?yaani ulitaka watu milioni 45 wote waongee wanataka nini?Nimekudharau sana!!!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
kwani utaratibu wa kuingia katika huo ukumbi wa ITV illi kuchangia upoje? Ni malumbano gani hayo ambayo wachangiaji wake wote wanafanana kifikra... hata uvaaji wa wachangiaji ulikuwa common isivyo kawaida kama vile walipewa maelekezo ya mavazi... serikali 3 inawezekana pasipo shaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…