ITV kipima joto:Rasimu ya katiba.Je inajibu matarajia ya watanzania kwa miaka 50 ijayo?

ITV kipima joto:Rasimu ya katiba.Je inajibu matarajia ya watanzania kwa miaka 50 ijayo?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Angalia ITV live muda huu ili ufuatilie mjadala huu.

Mgeni alieoko studio ni mjumbe wa tume.
 
Prof. Kabudi anatetea status quo. Pamoja na kuijua sheria lakini siasa zinamfanya ayumbe na kujaribu kupotosha watu.
Mihimili ya mahakama na serikali lazima kila mmoja ujitegemee bila kuingiliwa na mwingine. Hasa hili la raisi kumteua jaji mkuu halikubaliki na hata wakilipaka rangi kwa kiasi gani haikubaliki.

Pia nimegundua kuwa hii ni rasimu ya mtazamo wa wajumbe wa tume na si rasimu yenye maoni ya wananchi wengi wa Tanzania.
 
Nashangaa! Tume imetumia ghalama kubwa kukusanya maoni ya wananchi, lakini kwenye rasimu yamejaa mawazo na mtazamo wa wajumbe! Serikali tatu ni upumbavu uliokithili. 99.99% ya watanzania walisema madaraka ya raisi yapunguzwe,maoni haya hayajafanyiwa kazi. Tanzania ya leo ina wasomi, kwenye hii rasimu hakuna mgawanyo wa madaraka(DIFFUSION OF POWER). Kaskazini tutaanza kudai nchi huru kwa muktadha huu.
 
Tuna maprofesa majina, wanasifiwaaaaa,hakuna kitu wamefanya nini cha kukumbukwa? Hii nchi ina watu ambao ni myopia,vijana wamekuwa makupe! Je,tutafika?
 
Jibu N Kama ni Ndio , H kama Hapana na S kama Sijui.

Msiandike longolongo mingi.
 
Prof. Kabudi anatetea status quo. Pamoja na kuijua sheria lakini siasa zinamfanya ayumbe na kujaribu kupotosha watu.
Mihimili ya mahakama na serikali lazima kila mmoja ujitegemee bila kuingiliwa na mwingine. Hasa hili la raisi kumteua jaji mkuu halikubaliki na hata wakilipaka rangi kwa kiasi gani haikubaliki.

Pia nimegundua kuwa hii ni rasimu ya mtazamo wa wajumbe wa tume na si rasimu yenye maoni ya wananchi wengi wa Tanzania.

kweli mkuu.
 
Back
Top Bottom