Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Mimi ni mshabiki wa tamthilia za ITV Tangu imeanzishwa, walianza na "Egoli" Place of Gold, ndipo wakaja na "Isidingo" The Needy.
Kitu ambacho ITV imejijengea heshima kubwa, ni ile concistance yake, Isidingo ni saa 1:30 usiku. Kwa vile naipenda sana tamthilia ya Isidingo and I can't afford to miss it, kumenifanya niwe a very good father, kila saa 1:30 jioni lazima niko home, unless otherwise.
Ikitokea kwa sababu yoyote nimemiss episode ya jioni, kesho yake asubuhi saa 3:30 nitaangalia marudio nikiwa popote kupitia simu yangu kwa kutumia ile ITV online kwenye play store.
Kitu ambacho I never miss ni marudio ya wiki nzima, Jumamosi usiku kuanzia Saa 5:00 usiku, baada ya kumuangalia Zomboko na Hawavumi lakini Wamo.
Wiki hii nilikuwa busy hivyo sikuweza kuangalia Isidingo wiki nzima, hivyo jana jioni nikasubiri marudio ya wiki, hayakuwepo, bila hata scroll ya kuapologize.
Baada ya kukosa marudio ya jana marudio mengine ya wiki ni Jumapili saa 4:00 asubuhi. Muda huo ni muda wangu wa kanisani huwa nasali misa ya pili. Lakini kutokana na jana kutokuwepo marudio ya wiki, leo ilinibidi nijihimu kuamka saa 11:00 alfajiri kusali misa ya kwanza saa12:00 asubuhi hadi saa 3:00 ili saa 4:00 niangalie marudio ya wiki.
Ilipofika saa 4:00 kuwasha ITV, duh! Isidingo haipo! Kulikuwa sijui na likipindi gani, kwa vile nilipania Isidingo, hata wangeonyesha kipindi kizuri vipi, mimi bado ningeona ni likipindi tu!
Where is the ITV concistance? Ukiwa fan wa tamthilia fulani, unakuwa na addiction, ukikosa unapata withdrawer symptoms ya hasira na kukasirika, ingekuwa sababu ni live program, huwa tunaelewa na tunavumia, lakini kuondoa Isidingo kuweka recorded program yoyote, sio kututendea haki sisi watazamaji wenu watiifu.
Wito kwa menejmenti ya ITV, tunaomba mtutendee haki sisi watazamaji wenu, kipindi fulani kwenye series kisipokuwepo kwa sababu yoyote, tujulisheni kwa scroll.
Hata kama alipokuwepo Mzee alikuwa hafanyi lolote kwenye programming na scheduling, hatukuzoea kuona mambo kama haya, sasa kwa vile Mzee Mengi hayupo, halafu, yanatokea mambo kama haya, msitufanye tukaanza kumkumbuka Mzee Mengi, kuwa haya sasa ndio yanatokea kwa vile Mzee hayupo.
Japo baada ya hicho kipindi, Isidingo ilikuja kuonyeshwa, two episodes za mwanzo zilikuwa skipped, missing two episodes, is a big loss kwa mfuatiliaji wa haya makitu. Matatizo kama haya hakuna kabisa kwenye DSTV, kwa kutumia Explorer, unarekodi episodes zote na utaangalia at your own time, ITV hawana PVR, na kwenye DSTV hawapo, what a loss?
Msitufanyie hivi.
P.