ITV on Facebook naona kuna kitu

ITV on Facebook naona kuna kitu

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
1,883
Reaction score
1,482
Naona kuna wanakifanya kisomi sana, wanatupia nukuu za mh Magufuli za Kampeni ambazo zina ukakasi. Mfano mkichagua mpinzani mtajuta sileti maendeleo hapa. Nimefuatilia watu wanao komenti wapo very aggressive kwa Magufuli na 90% ya comments ni total Negative.

Hii ina maana gani, kiuandishi ITV wanatageti nini ku-express kitu ambacho wanatamani wakizungumze wao lakini mazingira yanawabana wanamtumia nukuu za mgombea kum-critisize kauli zake."Maendeleo ndugu zangu hayana Chama". Kingine ni kujaribu labda kumkumbusha kuwa ni miaka 20 tu tumekuwa na vyama vingi kama kuna majimbo mengii yapo hoi yapo na yalikuwa chini ya CCM.

Kifupi ndio nilivyoelewa, kwanini wanaweka vipande vyenye utata by the way naendelea kufuatilia kwa karibu mikutano yote. Naona CHADEMA wameanza kufanikiwa kuwatoa kwenye reli CCM, kuna hoja wanazitupa makusudi wakijua CCM watajibu kwa kupanic na kuacha kutangaza sera.

1.Mishahara...hii hoja imejibiwa kwa majibu mepesi sana na Magufuli.

2.Mifuko ya hifadhi za Jamii, fao la kujitoa, huu ni mwiba

3.Bima ya Afya sijui kama kwenye ilani ipo.

4.Wakulima kukopwa

5.Ajira.

Lissu alipiga hii misumali akijua lazima italeta shida kule, kafanikia. Ajira zimetangazwa juzi elfu13 za Walimu. Wakulima wa Pamba wameanza kulipwa juzi na Bima ya Afya imetangazwa juzi.

Kilichoniangusha ni wale waliokuwa wanasema kuwa mwaka huu Magufuli hakuna haja ya kampeni maana mambo mepesii siwaoni kabisaa. Bashiru kaanza kuwafokea akina Nape na Kigwangala, wamerelax baada ya kupitishwa bila kupingwa wanaacha kumuombea kura Rais wao.

Naona NEC na ZEC..wanapata kigugumizi kutoa maamuzi ya wagombea mamia wa Upinzani waliowekewa Pingamizi. ..sijui wanajadiliana na nani?....maana kama nikufuata sheria mbona ziko wazi...nao wanatutia mashaka.

Swala la Amani linazungumzwa sana ila kinafiki sana...wanataka kutibu Ugonjwa bila kujua chanzo chake...hakuna Kiongozi yoyote siwa Dini wala siasa anayetuambia tuitunze Amani isipotee anayetuambia kwanini Amani huwa inavunjika kipi kinasababisha..."that is definitely hypocritical statement". .

Minadhani Haki ikitendeka hakuna Mtanzania ataethubutu kuvunja Amani..labda awe na matatizo ya Akili.."psychiatric "..case...

any way tuombe Mungu atupitishe hili salama inshalah. ..

Chief..Kiswanta Comrade. .🤝🏻🤝🏻🤝🏻🤝🏻
 
Naonakunawanakifanya kisomi sana...wanatupia nukuu za mh JPM ....za Kampeni ambazo zina ukakasi....mfano...mkichagua mpinzani mtajuta sileti maendeleo hapa..!!!!
Hawana namna. Hizo ndiyo nukuu za John. Sasa watapata wapi nyingine?
 
Back
Top Bottom