SoC04 Iundwe kamati maalumu ili kuchochea Uongozi

SoC04 Iundwe kamati maalumu ili kuchochea Uongozi

Tanzania Tuitakayo competition threads

Omary 1998

New Member
Joined
Jun 20, 2024
Posts
3
Reaction score
3
MAWAZO YANGU JUU YA VIONGOZI WANAOCHAGULIWA NA WANANCHI.
Katika nchi yetu Kuna jopo kubwa Sana la viongozi ambao huingia madarakani kupitia kuchaguliwa na wananchi ambao viongozi hao ni wenyeviti wa vijiji, madiwani na wabunge . Viongozi hawa hushika madaraka wakiwa na jukumu kubwa la kuhakikisha wanaleta mabadiliko chanya katika maeneo Yao na taifa Kwa ujumla Kwakua ni muhimili muhimu Sana.

CHANGAMOTO NINAYOIONA KATIKA UTENDAJI WAO.
Changamoto kubwa ninayoiona juu ya viongozi hawa kunako utendaji kazi Yao ni kama zifuatazo;

a. Kipindi Cha uchaguzi wamekuwa wakiahidi mambo mengi Sana Kwa wananchi lakini miongoni mwao pindi wanapopata madaraka husau Yale waliyoahidi Kwa wananchi Bali hubaki wakijali maslahi Yao binafsi . Hali hii imekua ikichochea kudolola Kwa maendeleo katika kata na majimbo mengi kutokana na kutokuwa na viongozi wenye weredi katika utendaji wao.

b. Uwepo wa miongoni mwao kujihusisha na ubadhilifu wa fedha za uma zinazopelekwa katika maeneo Yao zenye Nia ya kuleta maendeleo bali miongoni mwao wamekuwa wakishutumiwa kujihusisha na kuhujumu pesa hizo na kujinufaisha wao binafsi . Hali hii imepelekea kuchangia Kwa kiwango kikubwa kuzorota kimaendeleo katika kata na majimbo mengi Sana kutokana na kuchaguliwa viongozi wasio sahihi.

c. Pia wapo baadhi Yao wamekuwa wakishutumiwa kuhusika katika migogoro mbali mbali inayotokea katika maeneo Yao kama vile migogoro ya ardhi. Hali inayopelekea kufifiza juhudi za serikali katika kuleta maendeleo chanya katika maeneo Yao.

JE, NINI KIFANYIKE KUTATUA CHANGAMOTO HII ?
Kwa upande wangu napenda kushauri ianzishwe kamati maalumu ambayo inawezajulikana kama TANZANIA POLITICIANS OBSERVERS (TPO) . Kamati hii inaweza kuwa kuanzia ngazi ya taifa hadi wilaya zote nchini.

JE, KAMATI HII IPATIKANE KUTOKA WAPI ?
Kamati hii inatakiwa isitokane na chama chochote Cha kisiasa Bali iwe ni kamati huru ambayo itakuwa Haina mafungamano na upande wa chama chochote kwa lengo la kuleta haki na uwajibikaji wenye tija katika taifa Hili .

MAJUKUMU YA KAMATI HII (TPO).
MAONI yangu ni kua napendekeza kamati hii iwe na majukumu yafuatayo;

a. Kunukuu na kuhifadhi ahadi zote zilizoahidiwa na wagombea wakati wa kampeni ili kuweza kufuatilia Kwa ukaribu ukamilishaji wa ahadi hizo pindi wanapokuwa mmadarakani Kwa lengo la kuhakikisha viongozi hao ndani ya miaka mitano wanakuwa ni wenye kuwatumikia wananchi ipasavyo.

b. Kuwakumbusha viongozi waliofanikiwa kuchaguliwa kunako juu ya ahadi walizoahidi kipindi Cha kampeni ili waweze kuzishughulikia ipasavyo Kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi.

c. Kufuatilia ukamilishaji wa ahadi zote zilizoahidiwa na wagombea wakati wa kampeni pindi wanapokuwa madarakani.

d. Kufanya tathmini ya utendaji wa Kila kiongozi Katika nyanja mbali mbali Kwa lengo la kuleta hamasa na uwajibikaji wenye tija katika maeneo husika .

e. Kila baada ya miaka mitano kamati hii itoe hati ya utendaji wa Kila kiongozi ikiwa kama kiongozi kafanya kazi Kwa ufanisi wa Hali ya juu basi atapewa hati chanya na ikiwa kiongozi atabainika kafanya kazi chini ya kiwango basi atapewa hati Hasi.

f. Kuandaa barua za mapendekezo juu ya kiongozi husika na kuziwasilisha kwenye kamati kuu ya chama chake ili kukishawishi kutomrudisha kiongozi huyo katika kinyanganyiro kingine ikiwa atabainika ana hati hasi ya utendaji au kumrudisha katika kinyanganyiro kingine ikiwa ana hati chanya ya utandaji.

NAMNA YA UTENDAJI WA KAMATI HII (TPO).
Napenda kushauri kua Kila baada ya miaka mitano kamati hii iwe inawasilisha hati ya utendaji wa Kila kiongozi ikiambatanisha na barua ya mapendekezo Kwa kamati kuu ya chama chake husika ili chama chake kiweze kutambua Kwa ufasa mwenendo wa viongozi wao na kuweza kufanya tathmini zaidi.

Pia nashauri kamati hii ikiwezekana iwe na mamlaka ya kukiruhusu chama husika kumrudisha kiongozi Katika kinyanganyiro kingine ikiwa atabainika ana hati chanya au kutoruhusu chama husika kutomrudisha kiongozi Katika kinyanganyiro kingine ikiwa atabainika ana hati hasi katika utendaji wake ndani ya miaka mitano.

FAIDA YA KUUNDWA KAMATI HII.
Kuundwa Kwa kamati hii kutaleta matokeo chanya katika taifa letu kama ifuatayo;
a. Kutachochea uwajibikaji wa viongozi wote wanaoingia madarakani kupitia kuchaguliwa na wananchi mana wakati wote watafahamu kuwa wanafatiliwa Kwa ukaribu.

b. Kutachochea upatikanaji wa viongozi wenye weledi wa Hali ya juu ambao wataokua tayari kuwatumikia wananchi ipasavyo Kwa Hali na Mali Kwa lengo la kuleta maendeleo katika maeneo Yao na taifa Kwa ujumla.

c. Kutachochea maendeleo yenye tija katika kata na majimbo mbali mbali katika nyanja mbali mbali kama vile kilimo, afya, elimu , uvuvi, nk.

d. Kutachochea kupungua Kwa ubadhilifu wa Mali za uma mana viongozi wataokua ni wenye kufuata kanuni ili waweze kutumukiwa hati chanya.

e. Kutachochea vyama vya siasa kuweza kufanya tathmini ya utendaji wa viongozi wao kwa urahisi zaidi na kuweza kupendekeza viongozi wenye weledi zaidi ili wakaingie kwenye kinyanganyiro kingine.

F. Itachochea upatikanaji wa viongozi ambao ni chaguo sahihi Kwa wananchi mana Kuna wakati vyama vya siasa vimekuwa vikipitisha wagombea ambao si wenye kuhitajika na wananchi , hivyo kamati hii itasaidia uondoaji wa tatizo Hili.
 
Upvote 3
mpaka sasa sijajua tz tunaenda wapi hatujui kutafuta tunajua kuomba omba na kukopa kopa ovyo na tukikopa hatujui kuvitumia
 
Back
Top Bottom