Muharram wa Pili
New Member
- Jun 2, 2024
- 3
- 0
Nafahamu ipo Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum ikishughulikia masuala mbalimbali yahusuyo jamii, jinsia za vijana wakike na wakiume, changamoto za wanawake na wanaume, wazee pamoja na makundi maalum. Liakini bado haitoshi wizara hii kubeba mambo yote hayo.
Taifa ni kizazi cha jinsia kike na kiume ambao hawazaliwi wakiwa wazee bali huanza wakiwa watoto na baadae vijana. Katika hatua hizo mbili za utoto na ujana ndipo hasa panatakiwa kuwekewa mkazo kwa maana ndio chimbuko la ongezeko la watu wa Taifa letu. Upo usemi usemao "samaki mkunje angali mbichi..".
Wizara ya maadili watoto,vijana na uzalendo kwa taifa. Ndio itakayo kuwa na jukumu la kuwalea, kuwalinda na kuwafundisha uzalendo kizazi cha taifa letu. Wizara itashughulika na matatizo yawahusuyo watoto na vijana moja kwa moja kufuatilia na kutatua changamoto zao na kuwajenga katika makuzi yenye maadili mema.
Watoto wa mwaka 0-3 wasimamiwe haki zao za lazima sio tu kutoka kwa wazazi bali mamlaka za serikali chini ya wizara hii. Wapo wazazi wamekuwa hawawanyonyeshi watoto maziwa yao ya asili kwa visingizio visivyo na mantiki kama kulinda urembo wao. Kwa kuwa watoto hawasemi ni wajibu wa serikali kuwasemea na kuhakikisha wanaipata haki hiyo. Kwa wazazi wanaofanya hivyo wapewa ushauri wakikaidi wachukuliwe hatua za kisheria.
Siyo tu hivyo Wizara kupitia wajumbe wa nyumba kumi kumi kama wawakilishi wao wanaweza kufuatili mienendo ya wazazi ambao hawako makini katika malezi ama mienendo yao binafsi inaathiri ukuaji wa watoto kama vile ulevi na kupigana. Hivyo basi serikali itachukuwa jukumu la kuwapokonya watoto na kuelekeza walelewe kwenye vituo maalum au kwa ndugu atakayepewa usaidizi kutoka serikalini.
Watoto wa umri 3-7 wizara kwa kushirikiana na wizara mwenza ya elimu iunde mtaala utakaowafundisha watoto tabia njema, wajibu wao kama watoto na mipaka yao. Kuheshimu watu wazima, kujitunza kulingana na jinsia zao, kuhakikisha wanatizama michezo ya luninga yenye maadili ya umri wao, adhabu ziwe za kitoto na sio kupigwa kama watu wazima. Waandaliwe kuipenda elimu na nchi yao.
Watoto wa umri 7-15 watoto wa kiume walindwe na propaganda za uhuru wa kijinsia na zaidi waelimishwe kujiamini na kuwa wakakamavu, ziundwe sera nzuri za kutambua uwezo wa watoto wa jinsia zote na kuendeleza vipaji vyao.
Katika umri huu hususan watoto wakike humendewa sana na mafataki wenye uchu wa ngono hivyo ziundwe sheria kali sio tu kusubiri tukio litokee bali za kuzuia matukio ya aina hiyo kutokea. Hapa wizara inapaswa kutilia mkazo na kutokomeza masuala ya ndoa za utotoni,mimba na kuahakikisha elimu inakuwa kipaumbele kwa watoto wa kike.
Kwa watoto wenye umri wa miaka 15 na kuendea ambao sasa rasmi watakuwa wanatambulika kama vijana katika taifa serikali na jamii inapaswa kuwalinda na athari za mihadarati na matumizi ya Madawa ya kulevya na pombe kali kwa kuhakikisha sheria ambazo hazimruhusu mtoto chini ya umri wa miaka 18 kutumia bidhaa kama sigara na pombe na michezo ya kamari zinafautwa kwa ukali na hatua stahiki za kisheria. Vijana wapelekwe kwenye mafunzo ya kizalendo na ujasiri ili kulitumikia Taifa lao.
Kuna mambo mengi ya ujumla ambayo ni muhimu kuyasema hapa ili yawe angalizo kwenye kulea watoto na vijana wa taifa hili. Mila na desturi ambazo ni hasi lazima zipigwe vita kama vile ukeketwaji kwa wanawake,mafunzo ya unyago kabla ya umri wa mahusiano, matumizi ya vifaa vya kiteknolojia kama simu na kompyuta bila kufuata mipaka.
Mazingira hatarishi ya vishawishi kama ujengwaji wa sehemu za starehe karibu na makazi ya watu. Serikali ikataze usajili holela wa makampuni ya kamari limekuwa janga linalolemaza vijana wengi kujishughulisha katika ujenzi wa taifa.
Lakini zipo baadhi ya mila na desturi zenye tija kwa malezi ya watoto na vijana kama vile majando kwa vijana wa kiume na wanawake waliokuwa kwenye umri wa kujitambua. Serikali kwa kushirikiana na asasi za kidini na kimila ziweke utaratibu mzuri ambao utakuwa ni elimu zaidi na sio vinginevyo. Miziki na sanaa nyingine ziwe zinazingatia malezi na kuacha kutunga tungo tata za matusi ambazo zinaharibu kizazi na mamlaka zikemee.
Wizara ya maadili, watoto, vijana na uzalendo inapaswa kuundwa ili iwe wizara ya kimkakati katika kuhakikisha taifa letu lina wapika raia wa baadae watakao kuwa na weledi na utambuzi wa miendendo ya taifa lao zaidi uzalendo. Chapisho langu hili likachochee hamasa kwa wadau mbali mbali watakao kuwa na mawazo chanya yakuona umuhimu wa kuwepo kwa wizara hii makhusi kwa watoto na vijana warithi wa taifa letu.
Ndimi wenu Muharram wa Pili.

Upvote
0