Iwe kasoma Kayumba au EMs bado mwanao ana nafasi ya kufanikiwa maishani ukizingatia malezi bora

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Siku za hivi karibuni kumeibuka mabishano makali kuhusu kusomesha mtoto St Kayumba (Govt schools) au English Medium (Private school).

Upande wa St Kayumba wana hoja na hata wa Private pia wana hoja. Binafsi msimamo wangu ni kila mtu asomeshe mwanae kulingana na uwezo wake wa kifedha.

Faida ya St Kayumba ni kutokuwa na gharama kwa sababu hakuna ada.

EMs faida yake kuu ni angalau kujua lugha kubwa yaa kimataifa yaani kiingereza.

Ikumbukwe Kiingereza ndo lugha kuu ya kibiashara duniani.

Msingi mkuu wa mtoto kufanikiwa maishani ni malezi ya wazazi/walezi wake.

Kinyume na hapo hata angesoma shule bora kiasi gani inawesa isisaidie. Mzazi hakikisha tangu anapata akili unamjengea mtoto msingi mzuri wa kimaadili ili uje umsaidie akiwa mkubwa na kuanza kujitegemea.

Hakikisha mtoto anafanya kitu sahihi katika muda sahihi. Kama anatakiwa kufanya kazi za nyumbani hakikisha anafanya haswa na sio kufuata huu upumbavu unaoendelea wa kusoma muda wote.

Inasikitisha kuona wazazi tunawalemaza watoto kwa kudhani kazi za mikono sio sehemu ya mafunzo ya maisha.

Zile wiki nne za likizo ukimpeleka mwanao kwenye project fulani akapiga kazi za mikono badala ya kwenda tuition itakuwa somo zuri maishani ambalo kamwe hawezi kulisahau.

Pia itamjengea kujiamini.

Kwa mfano mimi nilivyomaliza darasa la saba nilipewa kazi ya kupanda miti kwenye shamba la ekari moja alilokuwa kanunua baba.

Nilihangaika na ile miti hadi muda wa kwenda form one ulipofika. Nilivyomaliza form 4 nilikabidhiwa shamba la vitunguu kuanzia kuandaa shamba hadi kuvuna.

Nilienda form five nikitokea shambani direct. Hata baada ya kumaliza chuo pale home walinipa bustani ya mboga kuitunza.

Hayo mapito yote niliyopitishwa na mzazi wangu yamenijenga nijiamini na kufanya vizuri kwenye ajira niliyojiajiri na kuajiri wengine.

Baadhi ya watetezi wa St Kayumba wanadai hela ambazo ungelipa ada EM ungenunulia viwanja na kufungua biashara ili baadae mwano arithi.

Sio wazo baya ila linamfaa sana mtu asiye naa ndoto za mwanae kuja kufanya mambo makubwa zaidi. Kupitia elimu nzuri mwanao anaweza kufanya makubwa zaidi yako.

Benj Fernandes, Fred Vunjabei, Elon Musk, Bill Gates ni miongoni mwa mifano hai ya watu waliozaliwa na wazazi matajiri ila wakapita njia zao binafsi huku wakiwa naa elimu nzuri na kuwa matajiri kuliko wazazi wao.

Kumsomesha mtoto ili aje kukusaidia kwa kukupa hela ni upuuzi uliotukuka. Watoto wasio na malezi bora huku wakiwa na elimu duni huishia kuuza kila kitu walichoritjishwa.

Kuna toto la kichaga lilirithishwa chama likaja kuporwa na mnyampaa msomi.
 
Duuh kote Umenena vyema,hapo kwa kinyampaa umeonyesha picha ya kijani sana uliyonayo!
 
MADA NZURI.

Mimi Binafsi SijaOA Bado ila Nimeshajipanga Huko Mbele Nitakachokifanya kwa Wanangu.

1. Wanangu Wote Watasoma Shule za serikali.
2. Nitawasimamia Watoto Waibue Vipaji Vyao. ( Huwa Naamini Kila Mtu Amezaliwa na Kipaji )
3. Kama itatokea Mtoto Atakosa Kipaji Basi Akimaliza Chuo Nitampatia MTAJI.
4. Lastly Miaka Yote From Anazaliwa Mpaka Anamaliza Chuo Nitawatafutia Connections Mbalimbali.

NB: Huwa Nawashukuru Sana Wazazi Walivyonilea, I've Been a Very hard Worker.
 
100% right. Cha muhimu ishi tu vizuri na watu. Connection ni watu.
 
Back
Top Bottom