J. Mnyika: How and Why did you loose Ubungo 2005?

Mie namshauri mdogo wangu Mnyika Arudi amalizie shule Kwanza then 2010 aje apambane na John Mashaka
 
Yohana wa Mnyika,

Nikiwa ni mwananchi wa kule Kishapu, Kibugumo, Wami, Mpanda, Utete, Kiembe Samaki, na Micheweni, mwanchi wa kawaida ambaye angekuuliza hilo swali kuwa ilikuwaje ukapigwa ngwala nawe ukanipa kijitabu au ki-pamphlate eti nikasome badala ya wewe kuchukua muda kunieleza kwa ufupi kilichotokea na hata kama ni kukiri kupotea stepu, basi kura yangu umeshaikosa.

Kosa ambalo mnalifanya Chadema ni kuleta intellectualism kwa wananchi ambao shida yao kuu ni kujua kesho wataamkaje. Alot of Socrates, Plato and Aristotle, while what Tanzania at his minute before you become Chama Tawala needs a Sankara, Doe even Lenin simple ways to capture souls!

Badala ya kuwapa wananchi simple and clear information kuhusu chama chenu itikadi yenu, mnarudia yale makosa ya baadhi ya Wamishenari wa kwanza ambao walikataa Watanganyika wasiwe Wakristo mpaka waende mafundisho kwa miaka miwili.

Nyinyi kama chama, mnapaswa kuongea na kila mwananchi kwa lugha inayoeleweka, isiyo ya kisomi sana na hata mtangaze kwetu ni nini mtakachokifanya zaidi ya kuing'oa CCM Ikulu.

Natumaini unapokutana na wananchi wa kawaida, unachukua muda na kuweka baraza mithili ya Mzee wetu Ali Hassan Mwinyi, to level with your future constituence.

Kama mgombea na Chama chako, inabidi mtafute jinsi ya kuwanyang'anya majimbo CCM kwa kutumia japo neno moja kama CCM wanalolitumia kuwapiga ngwara- NYERERE!

Hivyo basi, nakuomba tena kwa lugha nyepesi sana utueleze ilikuwaje na kulitokea nini Ubungo 2005, ili upate kura yangu.😎
 

..mmesahau jinsi wamachinga walivyomtema Mrema baada ya mtu wa kwao kushinda tiketi ya CCM?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…