Jack Patrick kutupwa JELA miaka 10..!!

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
Duh! Habari mpya kutoka huko Hong Kong, China zinaeleza kuwa kama atapatikana na hatia ya kukamatwa na madawa ya kulevya ‘unga', modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick' atatumikia kifungo cha miaka kumi jela.

Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho kilikwenda kumtembelea Jack akiwa nyuma ya nondo baada ya kuruhusiwa kumuona tangu Machi mosi, mwaka huu, mwanamitindo huyo amekata tamaa na hana matumaini ya kutoka jela hivi karibuni.

"Aisee Jack Cliff anatia huruma sana, hana matumaini ya kutoka hivi karibuni na ana maumivu ya kupitiliza," kilisema chanzo hicho.
Mpashaji huyo alizidi kuweka wazi kuwa Jack anasema kuwa kesi yake ni ngumu na endapo atapatikana na hatia, basi atakumbana na kifungo, si chini ya miaka kumi, jambo ambalo limemfanya kudondosha machozi kila kukicha huku akituma salamu nyumbani kwao Bongo.



Jack alikamatwa na unga kilo 1.1 huko Macau, Hong Kong mwezi Desemba, mwaka jana ambapo sasa kesi yake itaanza kuunguruma Septemba, mwaka huu.
 
Ndio wajifunze sasa...wao siwanataka utajiri wa haraka...Na wanyongwe tu
 
Naruhusiwa kumuwekea dhamana?

"Nlikuwepo":bolt:
 
Si alikuaga anasema ana pesa??ziko wapi ajitolee dhamana na Jux waapiii hiyo ni laana ya mmewe!!
 
Kumbe anabahati. Miaka Kami tu? Nilifikiri wanakata shingo.
 
Huyu dada ana sura mbaya

Acha hizo bwana.. Hapo tunaangalia alichokifanya ila si kujifanya wajua hadi kuingilia kazi ya aliyemuumba na kuanza kukosoa kazi yake.

Sie tuendelee kujadili kosa alilofanya ila hayo mengine si vizuri.
 
Kesi kuanza kuunguruma Sept parefu...........

halafu zile pic zilizozaagaa kuwa ametoka zilikuwa ni uongo!!!!!
 
Anaumia nini sasa km alibeba sembe hakujua yatakayomkuta..hajui kupona ni bahati na keshapona mara ngapi mpk akazidi kunogewa na biashara. .40 yake ishafika atulie tuuu
 
Hivi, haruhusiwi kumtaja aliyemtuma? Kama atafungwa, huyo boss wa madawa atarecruit vijana wengine au sio?Vijana wataendelea kuangamia mpaka lini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…