Jackline Ngonyani: Nashauri mchakato wa Twiga Cement kuinunua Tanga Cement uanze upya

Jackline Ngonyani: Nashauri mchakato wa Twiga Cement kuinunua Tanga Cement uanze upya

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mhe. Jackline Ngonyani, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma

Mhe. Jackline Ngonyani, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma tarehe 04 Mei, 2023 alipata nafasi ya kuchangia suala la Tanga Cement na Twiga Cement wakati wa kuwasilishwa kwa hoja ya bajeti ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara iliyosomwa na Waziri mwenye dhamana Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji

"Twiga Cement wanataka kununua kiwanda cha Tanga Cement, endapo Twiga Cement wakinunua hisa za Tanga Cement, Twiga Cement watakuwa wanamiliki hisa karibu asilimia 68 za soko suala hili linakinzana na sheria ambayo Bunge imeitunga, sasa najiuliza kwanini serikali imedhamiria kuvunja sheria hii?" - Mhe. Jackline Ngonyani, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma

"Nashauri mchakato wa Twiga Cement kuinunua Tanga Cement uanze upya kwasababu kama mchakato huu ungeenda vizuri kusingekuwa na kelele nyingi zinazopigwa hivi sasa kuhusu mchakato huu" - Mhe. Jackline Ngonyani, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma

FvTMesqWAB8YK68.jpg
 
Wenzake washakula hela, ye sijui alikuwa wapi...

Game ndio imeisha hivyo..
 
Back
Top Bottom