Jackline Wolper Akubali Kuposwa, ila Masharti na Vigezo Kuzingatiwa

Jackline Wolper Akubali Kuposwa, ila Masharti na Vigezo Kuzingatiwa

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
BAADA ya msanii wa filamu hapa Bongo, Manaiki Sanga kutangaza nia ya kutaka kumposa mwigizaji Jacqueline Wolper, staa huyo ameibuka na kumjibu kuwa na yeye yupo tayari kama ataweza kutimiza masharti.

Jackline Wolper

Akizungumza na mwanahabari wetu, Wolper alisema katika mila za Kiafrika, posa haikataliwi, inatolewa na kisha inajadiliwa kwa hiyo kama Manaiki kajipanga, apeleke posa ikajadiliwe na wazee wake.

"Nimesikia habari za Manaiki kutaka kuniposa nikacheka sana kwa sababu yeye kama yupo tayari apeleke posa itapokelewa kwani siku zote vigezo na masharti huzingatiwa, afuate utaratibu tu," alisema Wolper.
 
unafikiri huyo utamchukua kwa pesa za kimandazi? uliza ma x zake wamefirisika sasa

Lakini si kuna habari iliwekwa hapa kwamba bibi yake alimuulizia kuhusu mtoto, jack akajisikia vibaya sana na akasema kuwa hajapata mwanaume, sasa kwa uhaba wa wanaume ulivyo unadhani mahali kubwa ni ishu kwa used?
 
Huyu si anakoboa wenzake? Sasa akiolewa mademu zake wataishije?
 
Lakini si kuna habari iliwekwa hapa kwamba bibi yake alimuulizia kuhusu mtoto, jack akajisikia vibaya sana na akasema kuwa hajapata mwanaume, sasa kwa uhaba wa wanaume ulivyo unadhani mahali kubwa ni ishu kwa used?

Ndugu yangu usipoteze rasilimali zako (hasa muda) kuwaamini bongo movie, wenzako hao 24/7 wapo location... kila wakat wanaigiza huenda hata hiyo story ya bibi sijui kitu gani nayo pia alikuwa anaigiza tu
 
Back
Top Bottom