Jackline Wolper angalia ya mbeleni

Hassan Mambosasa

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2014
Posts
3,359
Reaction score
4,528
AKILI IMEGOMA KUSHAWISHIKA


Nikimkumbuka vizuri ni msichana mrembo niliyekuwa napenda sana kazi zake za uigizaji, kapata umaarufu mkubwa sana kutokana na uigizaji na hata kuchukua vichwa vya habari kwenye magazeti mbalimbali kutokana na vitendo vyake.
Mara nyingine gazeti linamuandika tu kwakuwa kashakuwa na jina kubwa, alizidi kujijengea umaarufu kwa sana baada ya kuwa ubavu ubavu na Mbongofleva mmoja kisha baadaye wakamwagana na kubaki historia kuwa waliwahi kuwa wapenzi.

Miaka ilipiga hatua sana na hatimaye dada huyu muumini wa dini ya kikristo akabadili dini na kuwa Muislam baada ya kumpata Jamaa mwenye pesa sana na mfanyabiashara mkubwa sana Tanzania, maisha yake yakawa ni ushungi tu kipindi hicho yupo kwenye uchumba na jamaa. Mfungo wa mwaka huo alifunga vyema kasoma Quran vilivyo kwa msaada wa Sheikh aliyemuajiri kwa kazi hiyo. Akawa na jina la kiislam na magazeti yakawa hayamuishi kumuandika kwa mwenendo wake huo.
Swala kwenye mfungo wote hazikuwa zikimpita akiwa kwenye uchumba na jamaa huyo, siku zilisonga mbele akawa ameteka vichwa vya habari kwa mwenendo wake mpya hata watu wakasahau skendo zake za nyuma na kumpa heshima.

Loh! Salaleh! Siku zote ukitaka kumuona kinyonga anavyobadili rangi basi subiri uone akibadili mazingira au akikutana na hali nyingine. Yule jamaa mambo yakamuendea vibaya na akafilisika kabisa, baada ya kufilisika pesa mdada huyu hatimaye shungi alilitupa. Shahada aliyotoa akisilimishwa aliisaliti na jina alilopewa baada ya kusilimu aliliacha akarudia jina la zamani maisha yakawa yanasonga mbele. Watanzania walisahau hili kwakuwa ni kawaida yao kusahau mambo yakipita tu.

Mwaka huu 2015 alikuja na kioja kipya kabisa baada ya mheshimiwa fulani kupitishiwa mkasi, akaenda upande wa pili wa shilingi. Bibie alikuwa naye chama kimoja lakini alipohamia upande wa pili wa shilingi naye huyo kaenda.
Haikupita hata muda mrefu nakumbuka shamrashamra hizi pamoja na wawambaji ngoma kila mmoja kuvutia upande wake aliwahi kuandika kwenye ukurasa wake facebook alihongwa milioni 50 aje upande ulee akagoma. Sasa hivi nins uhakika hicho kitu kafuta kwenye ukurasa wake, ila ilimpa umaarufu sana
Watu wengi waliamini kuhusu hili ila hata hawakujiuliza kubadili dini kisa pesa na kubadili chama kisa pesa kipi kigumu? Kama aliweza kubadili dini aliyozaliwa nayo kisa pesa, je hicho chama kakijua alipopata umaarufu itashindikana vipi

Ukipata jibu utaona kabisa hapo alikuwa anawachota raia wasiojua kitu, ukiangalia ni msanii wa maigizo. Uongo huo naweza kusema atadanganywa mtoto mwenye akili isiyopevuka, hata kama ni propaganda arudi kwa wajuzi wake wakamfundishe tena .


Mwisho kabisa awe kama dereva wa gari kwenye mwendo kasi, asiwe na hesabu za kusimama mita mbili mbele awe na hesabu za kusimama mita kumi mbele baada ya gari kupunguza mwendo. Namaanisha hivi asiangalie hali ya kipindi hiki katika hayo maisha yake bali aangalie hali ya baadaye, mfano hao unaowazushia hiyo propaganda wakishinda halafu akiwa na shida atafanyeje? Haya ni maisha leo hii umewagawa watu kwa lengo fulani kesho kinakuja kile utafanyeje, sifa za muda mfupi ni majuto ya muda mrefu.

NI HAYO TU NENO SI SHERIA


#Mastermind
 
Mtoa mada Hahaah hhaa. Sipendi kabisa kutaja watu lakini mbona hayo Jackline Wolper ni madogo tu ? nakushauri basi angalau ungeanza na

-Diamond - jinsi anavyotumia umaarufu wake na kuzidhalilisha chupi za wasichana wa kitanzania.
-Aunty Ezekiel - huyu ni mkwe wa mtu na bado kazaa na mwanamume nje ya ndoa
-Wema Sepetu- huyu hata najisikia kichefuchefu kumtaja.
 

ila kati ya hao uliowataja hakuna aliyeandika alihongwa milioni 50 na si kweli
 
ila kati ya hao uliowataja hakuna aliyeandika alihongwa milioni 50 na si kweli




Bado tunasubiri hizo darasa duara zako za hao wengine niliokutajia! Ni sawa unapenda maadili mema au sio? Sasa ni bora ukaendeleza hizo darasa za maadili kote kote na si kwa wale wanaoonekana kama wako kwenye Mambadiliko pekee ndugu. Hivi aliekugusa ni Jacky pekee sio? huo utakuwa sio uadilifu hata kidogo ndugu.
 
Hongera sana mkuu kwa ushauri mzuri..
 
Haahhahaha.
We una lako jambo sio bure jack aanakunyima usingizi....utakua JUNAITHAR (Jennifer) muuza mkorogo maana kichambo alichokupa ukaona umfungulie thread
 
Njaa ilikuwa inamsumbua,we mpaka akawazima hela wakina nanilie wale!msamehe bureee
 
Ccm buana.!!
Ebu mwache mtoto wa watu.
El asiposhinda maisha yataendelea tu.
Btw unamfatilia sana una udugu naye??
 
Haahhahaha.
We una lako jambo sio bure jack aanakunyima usingizi....utakua JUNAITHAR (Jennifer) muuza mkorogo maana kichambo alichokupa ukaona umfungulie thread
Msome alama za nyakati, baada ya kupita uchaguzi. Mmelewa ninachomaanisha, sikutaka wasanii hawa watumike kupotosha watu. Karejea kule alipokataa milioni 50
 
mbna hujamshauri madam njaa....au unatafuta bwa......a
Ulitukana ila nimekusamehe..... Msome alama za nyakati, baada ya kupita uchaguzi. Mmelewa ninachomaanisha, sikutaka wasanii hawa watumike kupotosha watu. Karejea kule alipokataa milioni 50
 
Msome alama za nyakati, baada ya kupita uchaguzi. Mmelewa ninachomaanisha, sikutaka wasanii hawa watumike kupotosha watu. Karejea kule alipokataa milioni 50,
 
Upo kwenye list ya wasanii wanao lipwa na CCM, hayo ya Wolper yanakuhusu nini? Kama hijaridhika na posho uliyo pewa waambie tu wakuongeze.
Msome alama za nyakati, baada ya kupita uchaguzi. Mmelewa ninachomaanisha, sikutaka wasanii hawa watumike kupotosha watu. Karejea kule alipokataa milioni 50
 
Ulitemwa kwa ushamba wako,kale malimao!
Msome alama za nyakati, baada ya kupita uchaguzi. Mmelewa ninachomaanisha, sikutaka wasanii hawa watumike kupotosha watu. Karejea kule alipokataa milioni 50
 
Dah umekuwa mtabiri uliyoyasema yametukia
Yule dada ni maigizo hadi kwenye real life, niliwahi kusema hilo ila watu ushabiki uliwazidi. Mtafuta ugali yule, si utabiri ungetuliza akili ungeona hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…