sembo
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 4,350
- 3,451
Jackson Mayanja ambaye alizaliwa Julai 27, 1969 nchini Uganda.. ni kiungo bora kabisa kuwahi kushuhudiwa nchini Uganda [achana na kina Okwi].
Jackson Mayanja ni maarufu sana kwa jina la Mia Mia [100 percent] nchini kwao, ambalo alipewa wakati anacheza El Masri ya Misri mwaka 1992.
Jina hili lilitokana na kila alichokuwa akifanya uwanjani alikuwa hakosei.. Basi waarabu wakaona isiwe tabu.. wakawa wanamwita 100 percent].
Timu alizowahi kutumikia kama mchezaji ni;
1987: KCC
1992: El Masri ya Misri
1995: Esperance ya Tunisia
1996: Alirudi tena KCC ya Uganda, nakuiwezesha kutwaa ubingwa wa ligi msimu uliofuata.
2001: Nakumbuka Waganda walilia sana huu mwaka, kwani Jackson Mayanja "Mia Mia" alistaafu rasmi kucheza soka..
Jackson Mayanja "Mia Mia" pia kapiga mpira mwingi sana katika Timu ya Taifa (U23) ya Uganda na Timu ya Taifa 'Uganda Cranes'.
Baada ya kustaafu soka, aligeukia kazi ya ukocha, na baadhi ya timu alizofundisha ni;
2002: URA SC ya Uganda.
2004: Kiyovu Sportive ya Rwanda.
2005: KCC ya Uganda.
Timu zingine alizowahi kufundisha ni Timu ya Taifa (U23) ya Uganda, Timu ya Taifa 'Uganda Cranes', Kagera Sugar na Coastal Union.
Huyu jamaa tangu anze kucheza soka, amepata mafanikio lukuki, mfano;
1987: Ukiwa ni msimu wake wa kwanza katika ligi huku akiwa na miaka 18 tu, alitupia kambani goli na kuiwezesha KCC kutwaa ubingwa wa ligi.
1992: Alikua mchezaji wa pili kutoka Uganda kucheza soka la kimataifa.. Na hii ni baada ya kujiunga na El Masri.
1993: Baada ya kuonesha soka la kiwango cha juu kabisa, 'waarabu' hawakua na hiana wakampatia tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu.
1997: Alichaguliwa kua mchezaji bora wa Mwaka nchini Uganda, na hii ni baada ya kuiongoza KCC kutwaa kombe la ligi kuu.. baada ya kutupia kambani goli 18.
2003: Akiwa kama kocha, aliiwezesha URA kutwaa Super League.
Huyu ndiyo Jackson Mayanja "Mia Mia" ambaye kwa sasa ni kocha msaidizi wa timu bora kabisa nchini Tanzania, Simba SC 'Taifa Kubwa'.
SIMBA SPORTS CLUB, NGUVU MOJA.