Jacob Massawe asaini mkataba mpya Namungo FC

Camilo Cienfuegos

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2015
Posts
19,380
Reaction score
68,484
Jacob Massawe 33, nahodha wa Namungo Fc ya Ruangwa , Lindi amesaini mkataba wa mwaka mmoja kusalia klabuni hapo.

Mkongwe huyu amehudumu kwa muda sasa kwenye ligi kuu huku akiwa na kiwango kilekile.

Nahodha huyu wa Namungo ananikumbusha nahodha wa zamani wa Kagera Sugar, George Kavila ambaye yeye alicheza ligi kuu mpaka pale alipostaafu akiwa na miaka 41.

Mimi ni shabiki sana wa wachezaji wenye kujitunza na wasio na makeke wala show off.

Hongera sana Jacob Massawe
 
Una uhakika ana miaka 33?

Mwaka 2011 alikuwa mchezaji bora wa ligi kuu (MVP). Unataka kutuambia alikuwa MVP akiwa na miaka chini ya 20?, kumbuka kipindi hicho ili ucheze ligi kuu kwa ushindani lazima uwe na miaka walau 25 na kuendelea.
 
Hii sura siyo ya miaka 33, ni kama 45 hivi
 
Huyu si bure atakuwa na duka maeneo ya Uwanja wa Majaliwa!😎😎😎😎
 
Una uhakika ana miaka 33?

Mwaka 2011 alikuwa mchezaji bora wa ligi kuu (MVP). Unataka kutuambia alikuwa MVP akiwa na miaka chini ya 20?, kumbuka kipindi hicho ili ucheze ligi kuu kwa ushindani lazima uwe na miaka walau 25 na kuendelea.
Wabongo bhana, wewe ndio mamake, wewe kuballi alichosema yeye mwenyewe
 
Huyu jamaa anasema ameanza kucheza ligi kuu mwaka 2006.
 
Wabongo bhana, wewe ndio mamake, wewe kuballi alichosema yeye mwenyewe
Kuna mchezaji mmoja wa Afrika Magharibi, mama yake alifariki mwaka 1985 ila yeye kwenye vyeti vya kuzaliwa kaandika amezaliwa 1990, sasa hapo tumwamini mchezaji au tuamini uhalisia?
 
Una uhakika ana miaka 33?

Mwaka 2011 alikuwa mchezaji bora wa ligi kuu (MVP). Unataka kutuambia alikuwa MVP akiwa na miaka chini ya 20?, kumbuka kipindi hicho ili ucheze ligi kuu kwa ushindani lazima uwe na miaka walau 25 na kuendelea.
Huyu mwaka 2007 alikuwa anacheza UMISETA hapo Uhuru sec shinyanga miaka 33 nihalali yake labda kama wewe ni mama yake unataarifa zaidi. Kipindi cha kina Id mob , buluba sec , umiseta ilikuwa ya moto sana Shinyanga
 
Reactions: K11
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…