Jacqueline Wolpe na kashfa ya kumpiga mizinga ya pesa sana mchumba'ke Wastara.

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper amedaiwa kuwa na tabia ya kumpiga mizinga (kuomba fedha) mume mtarajiwa wa mwigizaji Wastara Juma, Mark Edi.


Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper.


Chanzo makini kilicho karibu na Mark ambaye ni mfanyabiashara mwenye maduka ya nguo jijini Dar, kimepenyeza habari kuwa, kabla ya kuanzisha uhusiano na Wastara, Mark alikuwa na uhusiano na Wolper lakini alimshindwa kutokana na tabia hiyo ya kupiga mizinga.

"Yaani Wolper ni balaa, anampiga sana mizingamizinga jamaa, mara anataka elfu 25, mara 30 yaani ni balaa tupu hadi ikafika steji Mark akaamua kumpiga chini na kutulia na Wastara," kilisema chanzo hicho.Staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma. Baada ya kugaiwa ‘ubuyu' huo sambamba na ushahidi wa SMS zilizoonesha Wolper akimuomba Mark fedha, mwanahabari wetu alimtafuta Mark ili kuweza kujua kama madai hayo yana ukweli ambapo alipopatikana alikiri na kudai amemchoka mwigizaji huyo.

"Daah! Umezipataje hizo habari? Ni kweli Wolper alikuwa mtu wangu lakini kwa sasa sina habari naye, ni mtu muongomuongo, mizinga kila wakati hadi nikaona bora niachane naye nitulie na Wastara," alisema Mark ambaye kwa sasa wanapika na kupakua na Wastara.

[
]Mwigizaji Wastara Juma, akiwa na mume wake mtarajiwa Mark Edi.
Jitihada za kumpata Wolper ili aweze kufunguka kwa upande wake hazikuzaa matunda kwani simu yake iliita bila kupokelewa, jitihada zinaendelea.
 
Wasanii wetu wanapenda kurithishana mabwana.

Nadhani wanahitaji elimu juu ya maambukizi ya VVU.
 
Sasa wolper nae hiyo mizinga ya kitoto mara elfu 25, 30 sasa alikuwa anaiganyia nini. Ndio maana alichokwa haraka. Angekuwa anapiga mzinga mmoja mkubwa halafu anatulia kbs ht miezi miwili kisha anaibuka na mwingine kwa strong point mbona kusingekuwa na shida.
 
Wastara nae ana mabwana wangapi yule mwenye nywele ndefu yupo wapiii!!!!
Hivi hiyo mizinga ya 25 na 30 ni kweli au udaku wolper au maana 30 haitoshi kabisaa japo hatuwatafutii tukawawekea mifukoni
Au umesahau zero nyingi nyingiii!!!😉😉😉😉
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…