Jadon Sancho ni mchezaji wa kiwango cha juu sana

Beira Boy

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2016
Posts
19,976
Reaction score
32,195

Jadon Sancho
Amani iwe nanyi wakuu,

Ukweli lazima usemwe. Jana ndiyo mara yangu ya kwanza kumshudia huyu kijana kutoka kwa Queen Elizabeth ukimutizama ni kama vile mlaini kumbe jamaa ni mapafu ya mbwa.

Akiwa na mpira huuchukui kizembe. Bado ana faida moja ya mbwembwe dah mshikaji ana mbembwe kinoma. Mara mpira auche mara aurudie yaan shida tupu. Bado anaweza piga mashuti kupiga vyenga bado anaweza kupambana kukaba.

Siyo wale madogo wa Chelsea urojo urojo. Dogo kama mount kila akipiga shuti lazima aunguke. Odoi legelege kinoma.
Abraham lege lege ile mbaya. Namtabiria kufika mbali huyu ninja wa kuitwa Sancho.

MUNGU AMABARIKI SANA

AMINA

LONDON BOY

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulichokishuhudia sijakijua. Jamaa ni mchezaji wa kawaida tu, Very Overrated English Player.

Nilichokishuhudia mimi ni kuwa Halland ni next big thing katika world of football

NA Dotmand wameramba dume kwa usajili wa Emre Can.
 
Umekosea bro mchezani hatazamwi kwa kufunga magori ya kuvizia

Mchezaji ni yule mwenye uwezo wa kumiliki mpira na kuuchezea anavyotaka

Kwa kifupi halland ni giroud aliyechangamka

Goli la Pili Lilikua ni world Class Strike. sijawahi shabikia masuala ufugaji magoli mengi kuwa ndio ishu kubwa, lakini kuna mambo yanakua siyo yakawaida.

Yule Sancho debe lote hilo unalolisikia ni kwakua Muengereza tu. Ila kwa kiwango chake wapo wingi mno anaofanana nao kiuwezo nawala hawatajwi tajwi kwa shangwe.
 
Bro mbona hoja zako zote umekazania uingeleza wa sancho?

Una shida gan na Uingereza wake?

Hizo chuki zako kwa Waingereza zitakuua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bro mbona hoja zako zote umekazania uingeleza wa sancho?

Una shida gan na uingeleza wake?

Hizo chuki zako kwa waingeleza zitakuua

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu pungumza presha. Kwa kifupi tu jamaa uwezo wake mdogo. Na ndio mana hata husikii timu za Real Madrid, Barca, Juventus, PSG kumuwania.
 
Haaland ni another level, dunia nzima inamuimba pamoja na kuwa timu ambayo sio maarufu sana duniani, this kid is amazing! amewafunika wote hakuna cha mesi wala ronado, ataweka rekodi ya dunia, mechi 9 magoli 12 UCL, magoli mengi kupita waliyofunga Barcelona msimu huu UCL!
 
Mkuu, kwa UCL amecheza mechi 7 na ametupia goli 10, japo hata hizo goli 10 ni zaidi ya zile ambazo Barcelona wamefunga msimu huu.
 
Ulichokishuhudia sijakijua. Jamaa ni mchezaji wa kawaida tu, Very Overrated English Player.

Nilichokishuhudia mimi ni kuwa Halland ni next big thing katika world of football

NA Dotmand wameramba dume kwa usajili wa Emre Can.
Nadhani utakuwa umelewa bro.
Hebu rudia tena?

English prayer lakini wajerumani wanamuamini na kumpa namba bado ni average?

Unajua takwimu zake zinasemaje?
Haland magoli anayofunga anayatoa wapi?
 
Tutajie hao wachezaji wengi wanaolingana kiwango na Sancho?
 
Ni wachezaji wawili tu sasa hivi ligi tano kubwa wenye double figure kwenye Assist na ufungaji. Messi na Sancho.
 
Kupigishana kelele na EPL fan boys ni kujisumbua tu. Ueleo wao katika ufahamu wa football ni zero kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…