Jaipur india: Hapa ndio 95% ya tanzanite ilipokuwa inauzwa

NEW NOEL

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2011
Posts
863
Reaction score
408


Kufuatia serikali ya tanzania kupiga marufuku usafirishaji wa madini ya tanzanite yakiwa ghafi nje ya nchi. Hali hii imesababisha maelfu ya watu waliokuwa wameajiriwa kama wafanyakazi katika viwanda vya kuzalisha madini ghafi ya tanzanite kukosa ajira. Na hata wale wafanyabiashara wa madini hayo kukosa mapato.

Ni katika mji wa Jaipur ambapo zaidi ya watu 30000,walikuwa wameajiriwa katika viwanda vya ku-process tanzanite ghafi. Lakini baada ya serikali ya Tanzania kuzuia usafirishaji wa madini hayo nje ya nchi,basi na viwanda navyo vimekosa masoko.
Mji huu wa Jaipur inaelezwa zaidi ya asilimia 95 ya tanzanite inayozalishwa mkoa wa manyara inapelekwa kule.
Kuzuiwa kwa Tanzanite kusafirishwa nje ya nchi na serikali ya Tanzania inafuatia kuanzishwa kwa sheria mpya ya madini ya mwaka 2010(mining act of 2010). Na kufuatia sheria hii mapato yanayotokana na madini haya yataongezeka maradufu zaidi.

Export ban on tanzanite in Africa leaves Jaipur gems sector in lurch - Times Of India

India tanzanite sector in crisis - National - thecitizen.co.tz


Sasa hivi mfanyabiashara wa madini anapotaka kusafirisha Tanzanite kwenda kuuza nje ya nchi anapaswa kuwa na certificate of origin.
 
sasa wao wanalalamika watu 30,000 kukosa ajira ya kuchonga mawe?
mbona hawaongelei Taifa letu lilikua linapoteza kiasi gani cha mapato muda wote huo? Kama vipi Jaipur ndogo ifunguliwe Arusha waje waombe vibali vya kazi tabu iko wapi?
 
inaonekana wahindi wamevuna miaka mingi sana hii tanzanite,hebu fikeni hapo nairobi mkajionee jinsi tanzanite inavyo pigwa mnada utadhani inachimbwa nchini kenya,hii nchi ufisadi hauwezi kwisha kama magamba watakuwa bado wanaongoza nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…