Jaja asaini miaka miwili Yanga

Rugby Union

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2012
Posts
402
Reaction score
252

Hatimaye mshamabuliaji Geilson Santos Santana "Jaja" raia wa Brazil leo amesaini mkataba wa miaka miwili (2014-2016) kuitumikia timu ya Young Africans kwa ajili ya michuano mbalimbali ikiwemo ya Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani.


Katibu mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu amesema usajli wa Jaja unakua ni wa pili msimu huu kwa wachezaji wa kimataifa baada ya awali kumsajili kiungo mshambuliaji Andrey Coutinho ambaye pia ni raia wa Brazil.

"Kazi yetu uongozi ni kutekeleza maelekezo ya kocha mkuu pamoja na benchi la ufundi, walitoa mapendekezo ya usajili kabla hawajaanza kazi na mengine baada kuwasili yote tunajitahidi kuyatekeleza ili kila kitu kiende safi" alisema Beno.


Jaja ambaye alizaliwa tarehe 21 Septemba 1985 na kukulia katika mji wa Aracaju nchini Brazili mpaka anasajiliwa na timu ya Young Africans alikuwa akiichezea timu ya Itabaina FC iliyopo nchini Brazil.

Mshambuliaji huyo mwenye mwili uliojaa vizuri tayari alishaanza mazoezi tangu katikati ya wiki iliyopita chini ya Kocha Mkuu Marcio Maximo na msaidizi wake Leonado Neiva ambao wanaendelea kukinoa kikosi cha Young Africans kwa ajili ya michuano mbalimbali.

Chanzo: Tovuti ya Yanga

CC: Makoye Matale
 
Last edited by a moderator:

Asante sana kwa taarifa. CC. Ivo Mapunda & Aishi Manula (Ole wenu mkutane na huyu jamaa).
 
the next four signings will be jeje, jiji,jojo & finaly juju
 
Hebu tupeni statistics zake.

Amecheza mechi ngapi,amefunga goli ngapi,ametoa assists ngapi,kadi za njano,nyekundu nk.
 
Kazi kwao wapinzani wakae mkao wa kuokota mipira wavuni..................
 
Hebu tupeni statistics zake.

Amecheza mechi ngapi,amefunga goli ngapi,ametoa assists ngapi,kadi za njano,nyekundu nk.

Sijui kama unaweza kuzipata maana hata aliyemsajili hana hizo takwimu.Kamati ya ufundi yenyewe hizo takwimu hawana iwe shabiki.
 
Hebu tupeni statistics zake.

Amecheza mechi ngapi,amefunga goli ngapi,ametoa assists ngapi,kadi za njano,nyekundu nk.

Ligi ikianza utakuwa unaandika hizo takwimu, mwisho wa msimu wa ligi utaziweka hapa ili tuzijadili. Kwa kuanzia andaa kalamu na daftari siku ya mechi ya ngao ya jamii. Napendekeza pia TBL waje na kale ka mechi ka nani mtani jembe tuone kama pale Msimbazi bado ni jembe au umebaki mpini tu.
 
Huyu Deo Corleone ashabikia vya nje, sasa sijui kiherehere cha nini na Soka letu butua butua. Maisha ya kike haya...

cc: Gang Chomba
 
Last edited by a moderator:
huyu mtupu kabisa wabazil wanakua na soko kubwa ulaya huyu hata uarabuni wamemshiti
 
Watani nawasubili uwanjani tu huku nje siwawezi, hebu ligi ianze tuone haya magalasa yenu yanafanya nini
 
Tupe feedback mkuu
 
Daah ila tumetoka mbali sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…