Mkuu hukumu mara nyingi huandikwa kwa mkono kwenye jalada la kesi husika.
Wakati anaandika hupitia muenendo wa kesi wakati ilipoanza hadi ilipofikia, muenendo wa kesi huwepo kwenye file husika hivyo hufanya ulinganifu na uchambuzi wa vifungu na pia huweza kurekodi case tofauti za rejea.
Kimsingi uandaaji wa hukumu huchukua muda kutayarishwa na hukumu inaposomwa mahakamani inakuwa ni directly kutoka kwenye file imeandikwa kwa mkono, hii ni kuiepusha hukumu kuvuja kabla ya muda.
Baada ya hukumu kusomwa na hatua kuchukuliwa file hupelekwa kwa katibu mahsusi kwaajili ya uchapaji.
Uchapaji unapokamilika nakala hurudishwa kwa hakimu/ jaji kwa ajili ya kuhariri makosa ya kiuchapaji na hivyo hurekebishwa palipokosewa na hukumu husainiwa na hakimu husika.
Nakala ya hukumu huombwa kwa barua ambapo hakimu akiridhia kuwa upatiwe utapatiwa pasipo kuilipia.
Kumbuka;Nakala ya hukumu hutolewa bure.