Maneno matupu hayavunji mfupa, maji moto hayachomi nyumba. Hivyo ndiyo ambavyo mimi ningemhukumu Lissu kwenye kesi yake hii kama ningekuwa Jaji aliyesikiliza kesi.
Mimi naweza kusema na kuagiza jambo, lalini msikiloizaji wa maneno/maagizo/hotuba yangu nae anao wajibu wa kujua, kutii sheria na mamlaka wakati wa kutekeleza tamko/maagizo yangu. Anayo hiyari ya kutekeleza au kuacha kutekeleza kwakuwa na yeye anapaswa kujua Katiba, sheria na taratibu zinasema nini kuhusu jambo analotaka kulitekeleza.
Je, Lissu aliposema atakwenda kuhamasisha uasi kisha yeye akabakia gerezani hayo siyo maneno matupu ambayo hayawezi kuvunja mfupa wa mtu?.
Binafsi, binafsi, binafsi wale waliokwenda kuchoma mali za umma na watu binafsi walikuwa ni watu wazima waliopasaswa kuwa na wajibu wa kuijua katiba, sheria na kutii mamlaka. Walikuwa na utashi wa kuyakataa au kuyatekeleza maagizo ya aina yoyote ile, hivyo waadhibiwe kama wao waliochoma na waliowawezesha kuchoma na wanufaika wa vurugu kama wakibainika.
Labda kesi nyingine ambayo haijafunguliwa bado, lakini kwa kesi hii ya sasa MIMI ningemwacha huru.