Jaji francis mutungi ateuliwa kuwa msajili mpya wa vyama vya siasa...tendwa kwa heri

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji Francis S.K. Mutungi kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa.

Taarifa iliyotolewa Dar Es Salaam leo, Jumatatu, Agosti 5, 2013, na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Ijumaa iliyopita Agosti 2, 2013.

Jaji Mutungi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Mhe. John Tendwa ambaye amestaafu Utumishi wa Umma kwa mujibu wa sheria.

Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mutungi alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu, DAR ES SALAAM.



Chanzo.
JAJI FRANCIS MUTUNGI ATEULIWA KUWA MSAJILI MPYA WA VYAMA VYA SIASA...TENDWA KWA HERI - GUMZO LA JIJI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…