Jaji jasiri aliyebatilisha uchaguzi wa urais Kenya

kanonb

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2016
Posts
391
Reaction score
328
Jaji jasiri aliyebatilisha uchaguzi wa urais Kenya

  • 2 Septemba 2017

View attachment 580744

Haki miliki ya picha EPA Image caption Jaji wa makama ya juu David Maraga na wenzake wanne wameweka historia kwa kubatilisha uchaguzi wa urais wa mwezi Agosti

Jaji wa makama ya juu David Maraga na wenzake wanne wameweka historia kwa kubatilisha uchaguzi wa urais wa mwezi Agosti.

Wakenya wamempongeza Jaji Maraga kwa kuwa jasiri kutengua uchaguzi wa mtu aliyemchagua rais Uhuru Kenyatta mbali na kurudisha imani katika idara ya huru wa mahakama.

Magazeti kadhaa ya Kenya yamemtaja jaji Maraga kuwa mtu wa maadili kutokana na hatua yake ya kuwa muumini shupavu wa kanisa la Seventh Day.

View attachment 580747

Aliripotiwa akiliambia jopo lililokuwa likimhoji kwamba iwapo atachaguliwa kuwa jaji mkuu nchini Kenya hatosimamia kesi siku ya Jumamosi , ambayo ni siku ya kupumzika kwa wanachama wa kanisa hilo.

Wengine wamedai kwamba huenda hii ndio sababu kikao cha kwanza cha kesi ya kupinga uchaguzi wa rais Uhuru Kenyatta kilianza mwendo wa saa moja usiku siku ya Jumamosi baada ya ya siku ya Sabato kuisha.

Haki miliki ya picha Twitter Image caption Matamshi ya Jaji Maraga

Imeripotiwa kuwa wakati alipokuwa akikaguliwa alikabiliwa na madai kwamba alikula hongo.

Aliwashangaza wengi kwa kutangaza katika runinga za taifa akiapa kwa kushikilia kitabu kitukufu cha Biblia kwamba hajawahi kuchukua hongo katika maisha yake.

Jaji Maraga mwenye umri wa miaka 66, alifuzu kama wakili miaka 40 iliopita kutoka chuo kikuu cha Nairobi kabla ya kuhudumu kama wakili wa kibinafsi.

Alichaguliwa jaji 2003 na kujiunga na mahakama ya rufaa 2012. Ameoa na ana watoto watatu.

Mwaka uliopita kufuatia kustaafu kwa jaji mkuu Willy Mutunga, aliwashinda majaji wengine 10, mawakili na wasomi kuteuliwa jaji mkuu.

Hatahivyo mapema mwaka huu aliripotiwa kumkemea mtu aliyemchagua, rais Uhuru Kenyatta.

Wakati akifanya kampeni nyumbani kwa jaji Maraga rais Uhuru Kenyatta alinukuliwa akisema kuwa wakaazi wa eneo hilo wanafaa kumpigia kura kwa sababu alimpatia kazi ''mwana wao''.

Hatahivyo jaji mkuu kupitia idara ya mahakama JSC alisema kuwa yeye sio mradi wa serikali.

Haki miliki ya picha EPA Image caption Jaji Maraga na wenzake katika mahakama ya juu nchini Kenya

Rais Uhuru Kenyatta hapo awali alikuwa amesema kuwa ataheshimu uamuzi wa mahakama , ijapokuwa alihoji ni kwa nini watu sita wanaweza kutoa uamuzi unaokwenda kinyume na matakwa ya Wakenya.

Hatahivyo baadaye alisema kuwa majaji hao walikuwa wamelipwa na ''watu wa kigeni pamoja na wajinga wengine''.

''Maraga na wahahalifu wake wameamua kubatilisha uchaguzi. Sasa mimi sio tena rais mteuliwa bali rais aliye mamlakani. Maraga anapaswa kujua kwamba sasa mimi ni rais anayehudumu''.

Licha ya vitisho hivyo , rais hana uwezo wa kumfuta kazi jaji mkuu ambaye muhula wake mmoja unakamilika wakati atakapofikisha miaka 70.

upload_2017-9-3_10-35-49.png
 
Jamaa kafanya kitendo cha kijasiri sana.. Uhuru Kenyatta nimesikia iwapo uchaguzi ukirudiwa na akashinda tena Anafumua system nzima ya mahakama
 
Tunahitaji katiba mpya itakayoweza kuwapa nguvu majaji wetu kuwa na mamlaka hayo
 
tushamwambia atakiona cha mtema kuni tukiingia ikulu "UHURU"
 
Jaji jasiri aliyebatilisha uchaguzi wa urais Kenya

  • 2 Septemba 2017

View attachment 580744

Haki miliki ya picha EPA Image caption Jaji wa makama ya juu David Maraga na wenzake wanne wameweka historia kwa kubatilisha uchaguzi wa urais wa mwezi Agosti

Jaji wa makama ya juu David Maraga na wenzake wanne wameweka historia kwa kubatilisha uchaguzi wa urais wa mwezi Agosti.

Wakenya wamempongeza Jaji Maraga kwa kuwa jasiri kutengua uchaguzi wa mtu aliyemchagua rais Uhuru Kenyatta mbali na kurudisha imani katika idara ya huru wa mahakama.

Magazeti kadhaa ya Kenya yamemtaja jaji Maraga kuwa mtu wa maadili kutokana na hatua yake ya kuwa muumini shupavu wa kanisa la Seventh Day.

View attachment 580747

Aliripotiwa akiliambia jopo lililokuwa likimhoji kwamba iwapo atachaguliwa kuwa jaji mkuu nchini Kenya hatosimamia kesi siku ya Jumamosi , ambayo ni siku ya kupumzika kwa wanachama wa kanisa hilo.

Wengine wamedai kwamba huenda hii ndio sababu kikao cha kwanza cha kesi ya kupinga uchaguzi wa rais Uhuru Kenyatta kilianza mwendo wa saa moja usiku siku ya Jumamosi baada ya ya siku ya Sabato kuisha.

Haki miliki ya picha Twitter Image caption Matamshi ya Jaji Maraga

Imeripotiwa kuwa wakati alipokuwa akikaguliwa alikabiliwa na madai kwamba alikula hongo.

Aliwashangaza wengi kwa kutangaza katika runinga za taifa akiapa kwa kushikilia kitabu kitukufu cha Biblia kwamba hajawahi kuchukua hongo katika maisha yake.

Jaji Maraga mwenye umri wa miaka 66, alifuzu kama wakili miaka 40 iliopita kutoka chuo kikuu cha Nairobi kabla ya kuhudumu kama wakili wa kibinafsi.

Alichaguliwa jaji 2003 na kujiunga na mahakama ya rufaa 2012. Ameoa na ana watoto watatu.

Mwaka uliopita kufuatia kustaafu kwa jaji mkuu Willy Mutunga, aliwashinda majaji wengine 10, mawakili na wasomi kuteuliwa jaji mkuu.

Hatahivyo mapema mwaka huu aliripotiwa kumkemea mtu aliyemchagua, rais Uhuru Kenyatta.

Wakati akifanya kampeni nyumbani kwa jaji Maraga rais Uhuru Kenyatta alinukuliwa akisema kuwa wakaazi wa eneo hilo wanafaa kumpigia kura kwa sababu alimpatia kazi ''mwana wao''.

Hatahivyo jaji mkuu kupitia idara ya mahakama JSC alisema kuwa yeye sio mradi wa serikali.

Haki miliki ya picha EPA Image caption Jaji Maraga na wenzake katika mahakama ya juu nchini Kenya

Rais Uhuru Kenyatta hapo awali alikuwa amesema kuwa ataheshimu uamuzi wa mahakama , ijapokuwa alihoji ni kwa nini watu sita wanaweza kutoa uamuzi unaokwenda kinyume na matakwa ya Wakenya.

Hatahivyo baadaye alisema kuwa majaji hao walikuwa wamelipwa na ''watu wa kigeni pamoja na wajinga wengine''.

''Maraga na wahahalifu wake wameamua kubatilisha uchaguzi. Sasa mimi sio tena rais mteuliwa bali rais aliye mamlakani. Maraga anapaswa kujua kwamba sasa mimi ni rais anayehudumu''.

Licha ya vitisho hivyo , rais hana uwezo wa kumfuta kazi jaji mkuu ambaye muhula wake mmoja unakamilika wakati atakapofikisha miaka 70.

View attachment 580750

Nadhani hii nguvu ya ' Kumsifia ' tungeihamishia katika kumuombea Ulinzi kwani kwa tunaojua tabia za ' Umafia ' za Uhuru Kenyatta kuna uwezekano mkubwa sana ndani ya hizo siku 60 ya marudio ya Uchaguzi tusiwe nae kama Binadamu hai huyo ' Jaji ' David Maraga. Uhuru ni ' Mafia ' mno na Mwalimu wake wa hii ' Kitu ' ni Marehemu Nicholas Biwott ( kafariki dunia mwezi May au June mwaka huu kama sijakosea ) ambaye ndiyo alikuwa ' King of Assassinations ' nyingi mlizowahi kuzisikia kutokea huko Kenya ambapo ' assignment ' yake ya Kwanza ilikuwa ni ' Kumua ' aliyekuwa Waziri na Kiongozi ' Kipenzi ' cha Wakenya miaka ya 90's Hayati Robert Ouko.
 
Ole wako, nchi, akiwa mfalme wako ni kijana, Na wakuu wako hula asubuhi!
Heri kwako, nchi, mfalme wako akiwa mtoto wa watu, Na wakuu wako hula wakati ufaao, Ili makusudi wapate nguvu, wala si kwa ajili ya ulevi.
 
Nadhani hii nguvu ya ' Kumsifia ' tungeihamishia katika kumuombea Ulinzi kwani kwa tunaojua tabia za ' Umafia ' za Uhuru Kenyatta kuna uwezekano mkubwa sana ndani ya hizo siku 60 ya marudio ya Uchaguzi tusiwe nae kama Binadamu hai huyo ' Jaji ' David Maraga. Uhuru ni ' Mafia ' mno na Mwalimu wake wa hii ' Kitu ' ni Marehemu Nicholas Biwott ( kafariki dunia mwezi May au June mwaka huu kama sijakosea ) ambaye ndiyo alikuwa ' King of Assassinations ' nyingi mlizowahi kuzisikia kutokea huko Kenya ambapo ' assignment ' yake ya Kwanza ilikuwa ni ' Kumua ' aliyekuwa Waziri na Kiongozi ' Kipenzi ' cha Wakenya miaka ya 90's Hayati Robert Ouko.
Tutajuaje kama Uhuru anatuzuga kwa kumponda jaji? Hili ni bara jeusi bana, kila kitu kiko organized, kwa misukule, mapembe or whatever. Kuna kitu walikiona mbele kama mkuu angepewa ushindi. Sasa wameiminisha dunia kwamba wao wanafuata demokrasia, subili mtiti wake baadae. Na hata huyo jaji anaweza kuwa sehemu ya mkakati. Achana na power mkuu. Sometimemes tunalishwa tu hata kama tunaona ni konokono, na tunasifia nyama tamu. Weee..
 
Back
Top Bottom