Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Dkt. Eliezer Fereshi ameagiza ngazi mbalimbali za mamlaka zinazohusika kufanya usuluhishi kuchukua hatua kwa watu au taasisi zinazopeleka kesi Mahakamani bila ya kuwa na ushahidi na kupelekea kuwepo kwa mahabusu wengi gerezani na kesi kuchukua muda mrefu.
Ameyasema hayo wakati akizindua jengo la mahakama ya wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma na kuongeza kuwa Mahakama inaendelea kuhakikisha wilaya zote nchini zinakuwa na majengo yake, kuongeza watumishi na vitendea kazi sambamba na kutumia teknolojia kurahisisha usikilizwaji wa mashauri.