Jaji Mkuu Kenya aondoa Sheria ya kuvaa wigi kwa Mawakili

Jaji Mkuu Kenya aondoa Sheria ya kuvaa wigi kwa Mawakili

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,711
Reaction score
35,644
Jaji Mkuu wa Kenya ameondoa sharti la Mawakili ambao wanajumuishwa rasmi katika kazi hiyo kuvaa wigi za kitamaduni, kwa sababu upatikanaji wake ni wa shida.

Wanasheria na Majaji nchini Kenya na nchi nyingine kadhaa za Kiafrika bado huvaa wigi nyeupe zilizosokotwa katika hafla rasmi, ambazo ni urithi wa ukoloni wa Uingereza.

Jaji Mkuu Martha Koome alisema Jumatano kwamba idadi kubwa ya mawakili waliorasimishwa katika sherehe rasmi ya kuwa mawakili wa mahakama kuu imekuwa changamoto kwao kupata wigi hiyo.

‘’Baada ya kuarifiwa kuhusu ugumu wa kupata wigi hilo kwa sababu ya idadi kubwa ya waombaji, ninaondoa hitaji hili kwa hafla hii,’’ alisema katika taarifa.

Alisema hata hivyo wale wanaotaka kuvaa vazi hilo bado wanaweza kufanya hivyo.

Zaidi ya mawakili 700 wanatarajiwa kuidhinishwa rasmi katika hafla itakayoongozwa na jaji mkuu siku ya Ijumaa.
 
Unapata wapi ujasiri wa kuandika uzi kama huu bila hata kapicha cha kunogesha uzi ?
 
Back
Top Bottom