Maneno mengi lakini hajatoa sababu za kimantiki kwa nini mahakama isiwe live.Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, George Mcheche Masaju, amesema kuwa shughuli za mahakama hazipaswi kuendeshwa kwa namna ya hadhara licha ya kuwa mahakama ni ya wazi, akibainisha kwamba zipo sheria maalum zinazoratibu mwenendo wa shughuli hizo.
Akihitimisha mkutano kuhusu ushirikiano na mahusiano katika utekelezaji wa majukumu ya utoaji haki uliofanyika Septemba 29, 2025 katika Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma, Jaji Masaju amesema:
“Mahakama siyo sehemu ya usikilizwaji wa hadhara. ‘Public hearing’ siyo ‘open court’. Kuna sheria zinazoratibu yanayoendelea pale. Wanaotaka kulazimisha kuingia mahakamani wakati hata nafasi haitoshi nao wajiangalie. Na wala hatuwezi kudai ‘live streaming’ au ‘live broadcasting’,” amesema.
Aidha, Jaji Masaju amebainisha kuwa ibara ya 18 ya Katiba ya Tanzania inaeleza juu ya haki ya kupata taarifa kwa kila mtu, lakini haimaanishi kwamba matukio yote yahusuyo mahakama lazima yatangazwe moja kwa moja.
Vilevile, amewatoa wasiwasi mawakili wa serikali akiwataka wasikae kimya kuhusu hoja za kisheria zinazohusu taratibu za mahakama, akisisitiza kwamba suala hilo halina sababu ya kuogopwa kulizungumzia hadharani.
Kauli hiyo imekuja wakati kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu, ikiendelea kusikilizwa mahakamani. Awali kesi hiyo ilikuwa ikirushwa moja kwa moja na vyombo vya habari, lakini baadaye urushaji huo ulisitishwa kutokana na pingamizi lililotolewa na mawakili wa upande wa serikali.
Kazi maalumu!Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, George Mcheche Masaju, amesema kuwa shughuli za mahakama hazipaswi kuendeshwa kwa namna ya hadhara licha ya kuwa mahakama ni ya wazi, akibainisha kwamba zipo sheria maalum zinazoratibu mwenendo wa shughuli hizo.
Akihitimisha mkutano kuhusu ushirikiano na mahusiano katika utekelezaji wa majukumu ya utoaji haki uliofanyika Septemba 29, 2025 katika Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma, Jaji Masaju amesema:
“Mahakama siyo sehemu ya usikilizwaji wa hadhara. ‘Public hearing’ siyo ‘open court’. Kuna sheria zinazoratibu yanayoendelea pale. Wanaotaka kulazimisha kuingia mahakamani wakati hata nafasi haitoshi nao wajiangalie. Na wala hatuwezi kudai ‘live streaming’ au ‘live broadcasting’,” amesema.
Aidha, Jaji Masaju amebainisha kuwa ibara ya 18 ya Katiba ya Tanzania inaeleza juu ya haki ya kupata taarifa kwa kila mtu, lakini haimaanishi kwamba matukio yote yahusuyo mahakama lazima yatangazwe moja kwa moja.
Vilevile, amewatoa wasiwasi mawakili wa serikali akiwataka wasikae kimya kuhusu hoja za kisheria zinazohusu taratibu za mahakama, akisisitiza kwamba suala hilo halina sababu ya kuogopwa kulizungumzia hadharani.
Kauli hiyo imekuja wakati kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu, ikiendelea kusikilizwa mahakamani. Awali kesi hiyo ilikuwa ikirushwa moja kwa moja na vyombo vya habari, lakini baadaye urushaji huo ulisitishwa kutokana na pingamizi lililotolewa na mawakili wa upande wa serikali.
Maneno mengi lakini hajatoa sababu za kimantiki kwa nini mahakama isiwe live.
Yeye mwenyewe ni zao la rushwa na upendeleo kwa hana huo uwezoMfumo wa Mahakama una matatizo makubwa kuliko matangazo live, ashughulikie rushwa, utoaji wa haki na kwa wakati sahihi kwanza
Mfumo wa Mahakama una matatizo makubwa kuliko matangazo live, ashughulikie rushwa, utoaji wa haki na kwa wakati sahihi kwanza
Tumewazidi ujinga na ulofa ndiyo maana tunaogopa ni aibu watu wanafungwa bila ushahidi hovyohovyo tu..vyombo vya habari vya televisheni viruhusiwe kuingia mahakamani.
..kama waandishi wa habari wa magazeti wanaruhusiwa basi na waandishi wa televisheni, au radio, waruhusiwe.
..suala la gharama sio la mahakama. Vyombo vya habari vitabeba gharama za kutangaza kesi ikiwa vitaona vinamudu kufanya hivyo.
..Mbona Kenya wameruhusu televisheni kutangaza kesi mbalimbali? Kenya wametuzidi nini Watanzania?
Hadi hapo sijasikia sababu ya msingi wa kesi kutoonyeshwa live.
Hii yote tunajua sababu ni kupooza upepo wa kesi ya Lissu kufanya live coverage katika kesi moja yenye maslahi ya umma inaghrimu kiasi gani?
Pesa wanazolipana kwenye posho , kununua magari na misafara kipi ni gharama?
Tunajua kapokea maelekezo kesi ya Lissu isiruke live maana siku ikiruka live basi itafunika matamasha ya wasanii ya Samia nchi ndio maana ukiangalia views za press za Polepole ni nyingi kuliko za matamasha ya Samia na kwa Polepole ni wanashindwa kuzuia badala yake wanakuwa wanaiblock YouTube.