Jaji Mkuu: Serikali inaingilia uhuru wa Mahakama

Jaji Mkuu: Serikali inaingilia uhuru wa Mahakama

FJM

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
8,081
Reaction score
6,200
JAJI Mkuu Mohamed Othman Chande, amekosoa mfumo wa kamati za maadili za mahakimu za mikoa na wilaya kuongozwa na wakuu wa mikoa, akisema kitendo hicho kinakwaza uhuru wa Mahakama.

Akizungumza katika majadiliano na ujumbe wa Mpango wa Hiari wa Kujitathmini Kiutawala Bora Afrika (APRM) jijini Dar es Salaam jana, Jaji Chande, alisema licha ya kuwepo kwa uhuru wa Mahakama, bado kitendo cha kamati za maadili za mahakimu kuwa chini ya viongozi wa Serikali, kinakwaza uhuru wa muhimili huo wa dola.

“Uhuru wa Mahakama ni suala muhimu katika kutekeleza kazi zake, nchi nyingi za Afrika zimeshafikia uhuru huo, hata hapa kwetu lakini kuna suala moja tu ambalo linatukwaza.”

Aliongeza; “Kuwepo kwa viongozi wa mikoa na wilaya kwenye kamati za maadili za mahakimu, inapunguza uhuru wa Mahakama. Ingefaa kamati hizo ziwe chini ya Tume ya Huduma za Mahakama.”

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Mathias Chikawe alipotafutwa kwa simu, ili kuzungumzia hoja hiyo ya Jaji Chande, hakupatikana licha ya simu yake kuita kwa muda mrefu.

Kwa upandeb wake Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani alipoulizwa kuhusu kauli hiyo ya Jaji Mkuu alisema; “Kamuulize mwenyewe (Jaji Mkuu Chande)… yeye si ndiyo amesema hivyo? Basi kamuulize yeye ndiyo anajibu,” alisema Kombani na kukata simu.

Kwa mujibu wa Jaji Chande, kamati hizo ngazi ya mkoa huwa chini ya Mkuu wa Mkoa na kati yake huwa Ofisa Tawala wa Mkoa huku mahakimu wakiwa wajumbe, huku katika wilaya pia Mkuu wa Wilaya huwa mwenyekiti na Ofisa Tawala akiwa katibu.

“Kila fani ina namna ya kuwajibishana. madaktari wana kamati zao, wanasheria wana kamati zao, basi hata sisi tuwe na chombo chetu,” aliongeza Jaji Chande.

Source: Mwananchi

Maoni yangu: Mh. Lissu alilisema sana hili bungeni. Lakini Mh Celina Kombani na mwanasheria mkuu Werema wakagoma kubadilisha. Wabunge wa ccm nao walipohijiwa na speaker walikataa hoja ya Lissu. Sasa Jaji mkuu amelisema, tena anawaambia watu wa nje ya nchi! Ni aibu kwa Tanzania!

Lakini jambo linalonistua ni majibu aliyotoa Celina Kombani alipopigiwa simu na mwandishi wa mwananchi! Kombani anasema " “Kamuulize mwenyewe (Jaji Mkuu Chande)… yeye si ndiyo amesema hivyo? Basi kamuulize yeye ndiyo anajibu" . Ingekuwa kwa nchi za wenzetu huyu mama angekuwa hana kazi kesho. Majibu gani hayo? Yeye ndiye aliyesimamia hii sheria mbovu, leo anataka jaji mkuu aulizwe nini? Na kama Celina Kombani hana majibu ya kwanini aliona inafaa mahakama kusimamiwa na wanasiasa wa ccm kuna sababu gani? Katiba inasema kuhusu separation of powers, Celina Kombani haelewi hilo?
 
Nakumbuka baada ya legal wrangle na lisu na AG,pinda akamuunga mkono lisu na hakuunga mkono hili suala
 
“Kila fani ina namna ya kuwajibishana. madaktari wana kamati zao, wanasheria wana kamati zao, basi hata sisi tuwe na chombo chetu,” aliongeza Jaji Chande.
...Huo ndio ukweli wenyewe. Hawako huru, ila, ni juu yao wenyewe kuamua.

...Siku ile -hao jamaa walipo lumbana bungeni- nilijiuliza kama mwanasheria mkuu anakumbuka dhana ya uhuru wa mahakama na ile ya good governance.
 
Nakumbuka Werema alimtupia vijembe lissu pale alipohoji kuhusu hili swala lilalozungumziwa na jaji mkuu.
maswala kama haya ni yakushtaki kwenye mahakama za wapiga kura ili ukweli uambatane na maamuzi magumu. :fencing:
 
Nakumbuka Werema alimtupia vijembe lissu pale alipohoji kuhusu hili swala lilalozungumziwa na jaji mkuu. maswala kama haya ni yakushtaki kwenye mahakama za wapiga kura ili ukweli uambatane na maamuzi magumu. :fencing:
...Wabunge huchangia makosa mengi ya kiufundi kufanyika, kwa kuendekeza ushabiki na kuweka maslahi ya nchi pembeni. Hawajui kuwa wanatengeneza mfumo utakaoshindwa kufanya kazi kwa ufanisi. Baadae watarudi bungeni kulalamika na kukosoa watu wasio na makosa, chanzo cha tatizo kikiwa wao wenyewe.
 
Ndiyo maana tunapodai katiba yenye tija kwa Taifa letu ni pamoja na mambo kama haya. Kama tutaendelea kuweka itikadi zetu mbele na kuweka utaifa wetu pembeni tutajikwamiha mengi sana.
 
JIngekuwa kwa nchi za wenzetu huyu mama angekuwa hana kazi kesho. Majibu gani hayo? Yeye ndiye aliyesimamia hii sheria mbovu, leo anataka jaji mkuu aulizwe nini? Na kama Celina Kombani hana majibu ya kwanini aliona inafaa mahakama kusimamiwa na wanasiasa wa ccm kuna sababu gani? Katiba inasema kuhusu separation of powers, Celina Kombani haelewi hilo?
Kwani Celina Kombani ndie alitunga hii sheria? Nilidhani bunge ndio linatunga sheria.

Na Chande nae mnafiki, kwa nini hakuongea wakati mjadala wa kitaifa unaendelea kabla ya sheria kutungwa na bunge?
 
Ndiyo maana tunapodai katiba yenye tija kwa Taifa letu ni pamoja na mambo kama haya. Kama tutaendelea kuweka itikadi zetu mbele na kuweka utaifa wetu pembeni tutajikwamiha mengi sana.
...Katiba mpya sio "mwarobaini" wa matatizo yetu!.

...Tunahitaji a change of mind sets, na tuache kufanya siasa kuwa chanzo rahisi cha mapato na kuficha uhalifu.
 
Kwa upande wake Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani alipoulizwa kuhusu kauli hiyo ya Jaji Mkuu alisema; "Kamuulize mwenyewe (Jaji Mkuu Chande)… yeye si ndiyo amesema hivyo? Basi kamuulize yeye ndiyo anajibu," alisema Kombani na kukata simu.

Majibu ya Waziri wa Sheria Tanzania huyo. Kwa Waziri tena wa sheria kutoa majibu kama hayo inasikitisha. Heri angekaa kimya tuu. Sijui ni lack of professionalism, siasa nyingi au ni dharau kwa waandishi wa habari?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Kwani Celina Kombani ndie alitunga hii sheria? Nilidhani bunge ndio linatunga sheria.

Na Chande nae mnafiki, kwa nini hakuongea wakati mjadala wa kitaifa unaendelea kabla ya sheria kutungwa na bunge?
CJ Chande ndiyo kwanza alikua amepokea ofisi,kama kuna watu wawili ambao wanastahili lawama ni jaji Augustino Ramadhan na AG Werema! Hawa jamaa wameidharirisha sana Mahakama kwasababu ya ukada wao kwa CCM! Usaliti wao utasimuliwa kwa vizazi.
 
Nakumbuka Werema alimtupia vijembe lissu pale alipohoji kuhusu hili swala lilalozungumziwa na jaji mkuu.
maswala kama haya ni yakushtaki kwenye mahakama za wapiga kura ili ukweli uambatane na maamuzi magumu. :fencing:

Viongozi wa Serikali ya Tanzania yaani kila kitu wao wanafikiria masuala ya Kisiasa tu; hivyo bila shaka hata kuongoza familiya zao pia huongoza kisiasa.

Wanashindwa kutofautisha masialahi ya Taifa na itikadi za Chama. Kila kinachohusu Serikali hata kama kina masilahi kitaifa basi lazima Wabunge na Watendaji wa Serikali watapinga kwa nguvu zote.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Tundu Lissu aliwatahadhalisha Bungeni Sitta na unafiki wake wakambeza
 
Kwani Celina Kombani ndie alitunga hii sheria? Nilidhani bunge ndio linatunga sheria.

Na Chande nae mnafiki, kwa nini hakuongea wakati mjadala wa kitaifa unaendelea kabla ya sheria kutungwa na bunge?

Mkuu Taso, Celina Kombani ndiye mwenye dhamana ya wizara iliyoandaa huo muswada/sheria. Na ni Celina Kombani ndiye aliyewasilisha muswada bungeni pamoja na kuutetea licha ya makosa makubwa kama haya yaliyosemwa na Jaji Mkuu.

Sijui kama ulifuatilia mjadala bungeni lakini hoja za Lissu akiungwa mkono na Zitto zilikuwa kali sana. Hili ni doa kubwa kwa mahakama kusimamiwa na wakuu wa wilaya/mikoa? Inavuruga kabisa dhana nzima ya utawala bora lakini pia ni kinyume na katiba - separation of powers.
 
Mkubwa FJM, alichofanya Kombani ndivyo mihilimi ya dola inatakiwa kufanya kazi, kila upande kuvutia ngozi kwake, ndio unapata mizani na uhakiki. Nategemea waziri atetee kwa nguvu mapendekezo ya wizara, nategemea Bunge lihakiki na kudodosa kila kinachopendekezwa kwa jicho la shaka na umakini, na nategemea mahakama nayo ifanye kila iwezavyo kulinda maslahi ya utoaji haki, hapo ndio tunapata mfumo thabiti wa ukaguzi na uwiano.

Bunge lilikuwa lina wajibu wa kutunga sheria bora, sio Celina Kombani. Na Chande aache unafiki wa kuongea wakati madhara yemeshafanyika.
 
Tatizo jingine ni kwamba miswada inapelekwa bungeni huku ikiwa imeandikwa kwa lugha ya kiingereza!
 
Hili suala linanikumbusha jinsi Tundu Lisu alivyotumia muda na weledi wake mwingi kulizungumzia hili na kuishiwa kupingwa na kuonekana hakuna analolijua. Hongera Lisu kwa lile ulilolifanya japo wengine ndo wanashtuka wakati huu kwani nakumbuka ulipingwa mpaka na mwanasheria mkuu wa serikali ambaye ni jaji kitaaluma!
 
Back
Top Bottom