Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Upande wa mlalamikaji ulieleza mahakama kwa ushahidi na facts kwamba mashtaka yaliyowasilishwa na Jamuhuri hayapo au hayana nguvu na msingi wa kisheria. Jaji alinaza baada ya kusikiliza pande zote mbili alikubali kuwa hati ya mashtaka ina makosa lakini pamoja na kubaini makosa kwenye hati ya mashtaka hakutaka kuifuta kesi.
Kitendo Cha kukubali kwamba mashtaka yamekosewa lakini hapohapo akaielekeza Jamhuri ikaandae mashtaka upya kilileta picha kwamba yeye Jaji anajua mashtaka sahihi ya mtuhumiwa kitu ambacho nikinyume kabisa na sheria. Jaji apaswi kuelekeza jamhuri ikatafute makosa maana kama Jamhuri ingelikuwa na makosa sahihi walipoletewa pingamizi walipaswa kukubali kwamba hati ina mapungufu na waje na chaji nyingine.
Kama katika kipindi chote Cha uendeshaji mashtaka Jamhuri haikuwahi kuomba ikabadilishe hati ya mashtaka, jaji Elinaza aliielekeza Jamhuri ikarekebishe vipi hati ya mashtaka? Mazingira haya ya Jaji kujielekeza kutoa maamuzi ya hoja kinyume na utaratibu ndiyo yaliyopelekea Mtuhumiwa Mbowe kumwomba ajiondoe.
Je, jaji mpya anakuja kutolea maamuzi hoja za ubovu wa hati ya mashtaka au anakuja kufanya kazi gani? Kama anakuja kuendelea na ushauri wa jaji aliyepita kwa Jamhuri nini nafasi ya Malalamiko ya Mbowe kuhusu maamuzi mabovu yaliyotolewa na Jaji Elinaza?
Ni sahihi kwa mahakama kuelekeza Jamhuri namna yakuandaa mashtaka? Endapo Jamhuri itaelekezwa na Mahakama namna yakurekebisha hati ya mashtaka, je jaji atakapofika hatua ya kutoa hukumu atapingana na ushauri alioutoa?
Maana kitendo Cha jaji kuielekeza Jamhuru ikarekebishe hati ya mashtaka kinaashiria kwamba mahakama tayari inayajua makosa ya mtuhumiwa na imeshajiridhisha kuwa makosa yalitendwa ila tu Jamhuri ilikosea kuyaandaa mashtaka hayo kwa ukakasi huu tutegemee mahakama kutoa Haki wakati imejipa kazi yakushauri mashtaka yaweje?