Jaji Mwalusanya atunae tena.

Jaji Mwalusanya atunae tena.

mayenga

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2009
Posts
4,118
Reaction score
1,970
Ndugu wana Jf,

Taarifa kutoka Dodoma zinasema kuwa Jaji mstaafu wa mahakama kuu,Mwalusanya amefariki Dunia na kuzikwa jana hukohuko Dodoma.

Jaji Mwalusanya atakumbukwa kwa mambo mengi hasa kesi yake maarufu ya MBUSHUU dhidi ya JAMHURI ambapo alionyesha msimamo wazi kwa kuipinga hukumu ya kifo.Jaji huyu ameandika kesi nyingi nzito na alijulikana kama Jaji mpigania haki.Hadi kifo kinamkuta licha ya maamuzi yenye kuwajali wanyonge ameandika machapisho mbalimbali kuhusu sheria za kazi,haki za wajane nk.

Mungu amlaze mahali pema.
 
Nimestushwa na kifo chake.
Aliifanyia mengi mazuri kada ya sheria nchini.

Mungu awafariji wafiwa
 
Rip Mwalusanya, ulikuwa Jaji mahiri na jasiri

Mhh Mwa Mwa ...maarufu mbona wanaondoka sana safari hii.
 
Huyu jamaa alikuwa mfano wa kuigwa na majaji wengine Tanzania! Kesi ya Mgombea binafsi ingekuja mbele ya Jopo la Majaji na yeye akiwemo kungekuwa na dissenting judgment!
 
Back
Top Bottom