TANZIA Jaji Samuel Victor Gibson Karua afariki dunia

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Familia ya Jaji Samuel Victor Gibson Karua Kwa masikitiko makubwa inawatangazia ndugu, jamaa na marafiki, Kifo cha mpendwa wao Jaji Samuel Victor Gibson Karua kilichotokea leo tarehe 26/02/2021 saa moja na nusu asubuhi (1:30) asubuhi, katika hospitali ya Saifee.

Msiba utakuwepo nyumbani kwa marehemu Jaji Samuel Victor Gibson Karua Kijitonyama. Ndugu wapendwa kutokana na janga linaloendelea hivi sasa ,familia inawapenda sana ila tunaomba kwa sasa familia pekee ndio ijumuike hapa nyumbani Kijitonyama na kuwaomba ndugu, jamaa na marafiki tujumuike pamoja siku ya jumatatu kwa ajili ya kumuaga na mazishi yatakayofanyika siku hiyo nyumbani kwake Goba Michigani pia tunasisitiza uvaaji wa barakoa na kunawa mikono na kukaa mbali mbali.

Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa, Jina lake lihimidiwe.

Familia ya Jaji Samuel Victor Gibson Karua.

======


Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Samwel Karua amefariki dunia leo Februari 26 katika hospitali ya Seifi iliyopo Oystebay jijini Dar es salaam.

Msiba upo nyumbani kwake Kijitonyama na mipango ya mazishi itajulikana hapo baadaye.

Mahakama ya Tanzania inatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia msiba huu.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.
 
Pole kwa familia, ndugu, jamaa na wote walioguswa na msiba huu.

R.I.P Jaji Karua
 
Kapicha tafadhali mleta uzi, ili na wengine tumfahamu zaidi
 
Inna lillah wainna ilaihyi rajiun.
Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa Amani.
 
Pole sana wafiwa How Old was He ?

Isije kuwa ni muendelezo wa kupoteza hazina ya wazee wetu
 
Tunapeleka Soko Matola, Mtaa wa Nonde nyumba namba sita au tutazika hukuhuku Kijitonyama?
Your browser is not able to display this video.
 
Kwa kuzingatia hali halisi serikali yetu ya wanyonge imeamua kuwekeza kwenye kuanzisha plant kubwa zaidi ya Nyungu Afrika mashariki na Kati ambayo ipo ndani ya hospitali kuu ya Taifa. Mradi huu unatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni na utaanza kufanya kazi haraka iwezekanavyo.πŸ‘ŠπŸ‘ŠπŸ‘Š Mitano ten
 
... Idara ya Mahakama miongoni mwa maeneo yaliyoahirka sana na Covid-19 na sekta ya elimu ya juu; maprofesa wamepigwa sana na Corona. RIP.
 
Kwa tutakao olewa mwaka huu ukikuta familiya ina wakwe mshukuru Mungu.

R.I.P Mh jaji.
... hakika umenena! Ndani ya kipindi cha miaka kumi ijayo mahari nyingi zitapokelewa na wakaka na kuolewa mtakaribishwa kwenye boma na mashemeji na mawifi no baba/mama mkwe! Wazee wanaisha!
 
RIP JUDGE SAMUEL VICTOR GIBSON KARUA

JAJI MSTAAFU WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA MHE. SAMWEL KARUA AMEFARIKI DUNIA

26-02-2021 0


Published By:LYDIA CHURI

Source: JAJI MSTAAFU WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA MHE. SAMWEL KARUA AMEFARIKI DUNIA
Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Samwel Karua amefariki dunia leo Februari 26 katika hospitali ya Seifi iliyopo Oystebay jijini Dar es salaam.
Msiba upo nyumbani kwake Kijitonyama na mipango ya mazishi itajulikana hapo baadaye.
Mahakama ya Tanzania inatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia msiba huu.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE
 
... mradi mkuwa zaidi wa sauna duniani uko Tanzania.
 

RIP JUDGE WILLIAM MAINA​

JAJI MKUU PROF JUMA AONGOZA KUAGA MWILI WA JAJI MSTAAFU WILLIAM MAINA​

24-02-2021 0





Published By:Mary C. Gwera


  • Ibada ya kuaga mwili yafanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Oysterbay
  • Mwili wake wazikwa katika Makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam
  • Jaji Maina atakumbukwa kwa Uadilifu, uchapakazi na uzalendo
  • Ibada ya kuaga mwili yafanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Oysterbay
  • Mwili wake wazikwa katika Makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam
  • Jaji Maina atakumbukwa kwa Uadilifu, uchapakazi na uzalendo
  • source : Judiciary of Tanzania | Home
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…