TANZIA Jaji Samuel Victor Gibson Karua afariki dunia

pole kwa familia na wafanyakazi wenzake.
hakika kifo ni funzo kwa sisi tulio hai,
tuache jeuri wala usimtedee binadamu mwenzio mambo mabaya, hakika hakuna atakaye ishi milele.
 
Jaji Karua alikuwa makini sana.
Nakumbuka akiwa Mahakama Kuu Mbeya aliwahukumu kunyongwa hadi kufa watu nafikiri wawili waliomuua kada wa CCM, na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rungwe, Nd John Mwankenja.
 
Si vyema kumsema marehemu, ila majaji wa WaTz wanatesa sana watu kwa ulaji rushwa, ooh Kijitonyama, mara Goba Michigani.., nyumba kila mahali
 

Apumzike kwa amani.

Familia kwa tahadhari yenu hakika bwana na akawalipe sawa sawa na kujali kwenu maisha ya watu.

Huku kwingine hadi pale ule mbuyu wenyewe wenyewe kabisa utikiswe, maisha yetu yanaendelea kuwa ni pata potea.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Si vyema kumsema marehemu, ila majaji wa WaTz wanatesa sana watu kwa ulaji rushwa, ooh Kijitonyama, mara Goba Michigani.., nyumba kila mahali

Kuliko polisi, tra, tume za uchaguzi, na hawa kina majiwe huko jikoni kwenyewe kabisa kabisa?

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…