Jaji warioba aficha maoni ya viongozi

Jaji warioba aficha maoni ya viongozi

ISMAIL MKIMBIZI

Senior Member
Joined
Jan 13, 2013
Posts
192
Reaction score
23
Kufuatia sakata la katiba mpya, Mwenyekiti wa tume ya Katiba Jaji Joseph Warioba ameacha kufafanua asilimia mbili za waliotoa maoni juu wa muundo wa muungano wamesemaje. Akifafanua umuhimu wa serikali tatu huku akishangiliwa na wabunge alisema asilimia 13 ya waliotoa maoni juu ya muungano walitaka serikali moja, 24% wakapendekeza seikali mbili na 61% wakapendekeza serikali tatu.

Ukipiga hesabu utaona jumla ni 98% ndiyo wamezungumziwa na 2% imefichwa ambapo wadadisi wa mambo wanasema hiyo ni sehemu ya viongozi wa ngazi za juu serikalini na wapambe wao walioagizwa kutoa maoni juu ya kuukataa muungano wa jinsi yoyote ili muungano uliopo uvunjike na kila nchi ijitegemee. Hii ni sumu ya hatari sana imo ndani kwa ndani!

Napenda kumpongeza kwa kazi ngumu aliyoifanya kukamilisha rasimu ya katiba, lakini napenda kuikosoa tume aliyoiongoza kuona kuwa katika kipindi cha miaka 50 iliyopita kumekuwa na faida kutokana na muungano huu tulionao ya kwamba umetuunganisha wananchi (Watanzania). Hiyo ni lugha ya kisiasa funika kombe mwanaharamu apite, ukiwapaka mafuta watanzania kwa mgongo wa chupa!

Haiwezekani kamwe hata kidogo na haiingii akilini Tume itueleze tuna faida ya wananchi kuungana kwamba " faida kubwa iliyopatikana katika miaka 50 iliyopita ni kuungana kwa wananchi" Iweje wananchi ambao ndiyo tunaunda serikali tuwe tumeungana harafu tuhitaji serikali tatu isiwe moja? Tena ikiwa tumeungana iweje tuhitaji serikali yenye misingi minne ya kiutendaji? Yaani Muungano wa hiari, ushirikiano, mshikamano na kutegemeana!

Kama kweli tunahitaji muungano wa hiari basi tukubaliane huu uliopo ni wa kulazimishwa! Kutembea na mwanamke kwa kumlazimisha sio mapenzi ni ubakaji ambapo ni kosa la jinai, hivyo hiyo faida aliyosema jaji Warioba kuwa watanzania tumeungana katika kipindi cha miaka 50 sio kweli bali ukweli ni kwamba tumevumiliana, hatujaungana na ndio maana kero zinazozungumzwa ni kigezo tosha cha kudhihirisha hili ninaloliamini.

Haiwezekani kuunganisha watu wenye tamaduni, imani, itikadi na malengo tofauti! Haiwezekani kufanya muungano wa Marekani na Iraq au Uingereza na Irani. Asilimia mbili iliyoachwa bila kutamkwa na Warioba imependekeza nini ndio hao wenye ushawishi mkubwa katika jamii ambao awali walishawishi kuwa muungano wa nchi moja kwa serikali mbili sio mzuri kwao wakapata muungano wa serikali mbili nchi mbili. Sasa baadhi yao wameshawishi muungano wa serikali tatu nchi mbili, wenye mamlaka tatu.

Fahari wawili hawakai zizi moja itakuwaje kwa fahari watatu? Kama kweli ni sawa ayasemayo Jaji Warioba kwamba faida kubwa iliyopatikana katika miaka 50 iliyopita ni kuungana kwa wananchi watanzania, asingependekeza muundo wa muungano wa hiari wa serikali tatu angefagilia 13% muundo wa serikali moja. Hizi lugha za kisiasa za kufunika kombe mwanaharamu apite zitatugharimu.

Iko siku hiyo 2% itahitaji kuvunja MUUNGANO WA TANZANIA itafanikiwa. Ilitaka serikali mbili nchi mbili ikapata na ikavunja katiba ya muungano wa Tanzania. Inahitaji serikali tatu, nchi mbili, mamlaka tatu huenda ikapata. Sintoshangaa kuona baada ya hapo changamoto zitazidi zilizokuwepo na kupelekea uvunjifu wa amani na kilio kitakuwa kikubwa zaidi kutaka muungano uvunjike na utavunjika! Vinginevyo DOLA itumie nguvu za ziada kuulinda muungano!
 
Aliona aina maana kuwazungumzia kwa sababu maoni yao yatakuwa ni kinyume na ya watu wanao waongoza
 
Jaji Wariobaaaaa!!!! Mzee umekuwa maji ya moto kila anayekugusa anaungua. Hongera sana mzee kwa kazi nzuri isiyo na upendeleo wowote. Historia mpya umeandika na itakukumbuka daima.
Ikiwa watu watapuuza maoni yako, wasije shangaa siku zijazo watu wakienda porini kuitafuta Tanganyika.
Inawezekana wakati huo ndiyo watu hasa wahafizina watakumbuka busara zako.
Ili kuepusha machafuko na keleleza wananchi ni busara wale wanaopinga kurejea kwa Tanganyika wakabadili msimamo wao. If not....nimenukuu mdau Bw/Bi. BAK aliyesema "Sijui hawa MACCM wana tatizo lipi la uwepo wa Tanganyika. Tumekuwa na Serikali mbili za Zanzibar na Muungano kwa miaka 50 sasa, kama wanataka Serikali mbili basi ziwe za Tanganyika na Muungano kwa miaka mingine 50 na hivyo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ipotee. Tuone kama hili litaridhiwa na Wazanzibar". Ila ikumbukwe kuwa tulikuwa na serikali mbili nchi moja, ila leo tuna serikali mbili nchi mbili ambalo ni kinyume na Katiba ya sasa.

Ni vizuri Tanganyika irudi ili tuheshimiane
 
Back
Top Bottom