Jaji Warioba: Ajira ni tatizo kubwa sana linalowakumba vijana wetu. Nashauri Elimu yetu iangaliwe upya!

Jaji Warioba: Ajira ni tatizo kubwa sana linalowakumba vijana wetu. Nashauri Elimu yetu iangaliwe upya!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Jaji Warioba anasema katika kipindi cha miaka 60 ya Uhuru wa nchi yetu bado Ajira kwa vijana ni tatizo kubwa.

Jaji Warioba ameshauri mfumo wa elimu uangaliwe upya.

CHanzo: BBC Dira ya Dunia!
 
Sahihi kabisa, kitu cha kwanza kujiuliza elimu ni nini, itamsaidiaje kijana kujitambua, kujitegemea, kujiamini, kutumia mazingira yake kupata kipato halali.

Kuwa na uwezo wa kujiajiri na kuajiri wengine na kuajiriwa.

Elimu ni kuyamudu mazingira yako.
 
Ukiangalia hata sera za serikali hii, ni watu labda waliosoma lakini hawakuelimika.

Vitu vya msingi kama demand and supply, inflation, elasticity, multiplier effects, umuhimu wa kilimo, gharama za mafuta (petrol, diesel) kwenye uchumi maisha ya Wananchi wote hawavijui au hawajali.
 
Kama corona na sasa OMICRON ndio kikwazo cha kupiga kura ya maoni, basi ikubalike kuwa yale yaliyomo kwenye rasimu ambayo hayana utata na hayahitaji ulazima wa kupigiwa kura basi yashuhurikiwe wakati huu bila kupoteza muda na hayo wengine yatashuhulikiwa hapo baadae!
 
Hapa anazungumzia ajira!
 
Mi napingana na kuwa elimu inayotolewa Tanzania ubora wake na mfumo wa ajira, shida iliyopo mfumo wa ajira ndio tatizo kubwa nchi yetu tunahitaji wawekezaji wa kutosha wafungue viwanda, migodi, mashamba makubwa ya mazao na mifugo hapo shida ya ajira itapungua.

Kuliko kutegemea serikali iwaajiri wananchi wake na mfano mzuri ni Kenya mzunguko wa pesa mkubwa sana viwanda ni vingi sana usipo ajiriwa nunua malighafi kauze kiwandani maisha yanasonga sasa shida bongo hata sehemu ya kwenda kuomba kazi huioni, unalima lakini pa kwenda kuuza mazao yako hupaoni tatizo linakuja hapo sasa hao wasomi walipata bahati ya kupata ufadhiri kwenda kusoma USA na UK wanaanza kuona elimu yetu bongo haitoshi.
 
Back
Top Bottom