Jaji Warioba atoa msimamo wake

Jaji Warioba atoa msimamo wake

Miwatamu

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2012
Posts
1,450
Reaction score
489
Jaji Warioba ameonesha kufadhaishwa na jinsi vyama vya siasa vinavyowalisha wananchi wake maneno ya kuongea katika kuchangia maoni ya muundo wa Katiba mpya. Amesema.......... "Sasa ninao uwezo wa kugundua kuwa haya ni maoni ya mtu mwenyewe au ametumwa"

Nahisi MaCCM hasira zinawapanda na kutamani kumtungua kwani inaonekana kama anawasaliti.

HONGERA JAJI, FANYA KAZI YA WANANCHI KWA MANUFAA YA NCHI.
 
ccm mavi yanawaumaa kuona babu Warioba kagoma kuburuzwaa.... !
kila siku natamko yasiyokuwa na tijaaa
 
huyu mzee ana msimamo sana juu ya mambo yake kwani hata kipindi chake cha utawala alikuwa haendeshi nakwawale wanao kumbuka hilo watakwambia juu ya G55
 
Aaah we hujamsikia akiuliza "mbunge wangu yuko wapi? Nilimtuma akawaambie wenzake (CDM) sitapokea maoni ya Helkopta"...?!!!!!
 
Nimependa jinsi mzee Warioba alivyoacha maslahi ya vyama (ukizingatia ni mwanaCCM) lakini haoneshi dalili za kuburuzwa na CCM. Kwanini wawakaririshe watu vitu vya kuongea? Hivi hao wanaokaririshwa wanajua athari zake?
 
Hakika warioba ni mtu wa pekee sana, anauwezo wakusema no kama jibu ni no. Nape atambue kuwa katiba tunayoitengeneza si ya CCM bali ni ya watanzania. Namkubali sana warioba kutambua mauni ya kukaririshwa na maoni ya wananchi halisi. Warioba tafadhali piga chini maoni yote ya kukaririshwa na chukua maoni halisi ya wananchi. Wananchi tunasema tunataka selikali tatu au moja tu, zaidi ya hapo hatutaki.
 
hawa akina waryoba walisha kula kiapo...awatabiriki hawa..ni ccm damu damu mpaka basi
 
Aaah we hujamsikia akiuliza "mbunge wangu yuko wapi? Nilimtuma akawaambie wenzake (CDM) sitapokea maoni ya Helkopta"...?!!!!!

ni kweli kabisa mkuu, tume haipokei maoni ya helkopta ndiomaana haikuwawahi kuandikwa kama sehemu maoni ya chadema.

Ila amesema ule mpango wa kuandika waraka na kuwapa wanachama kuusoma kama maoni hautakiwi na tume kabisa, na kuna mpango maalum wa kuyatazama haya maoni na kuchuja yale maoni ya raiya na kutupilia mbali yale yakukaririshwa na Nape Nnauye.
 
Last edited by a moderator:
Kinana, Nape, Mwingulu, Kikwete, Shein, Nahodha na Vuai wote ni akili mgando wana fikra zile zile za miaka 100 iliyopita
 
Mzee Warioba katumia falsafa ya juu, kwa watu wenye akili za haraka haraka watajua ni helkopta ya CHADEMA.
Jamani ikumbukwe kwamba CCM ndo wametoa mpaka waraka na kuwakaririsha wajumbe wao ili wapinge serikali tatu. Sasa kumekucha. Mzee Waryoba tunakuamini, tunakutegemea kwamba kwa zaidi ya miaka 50 ijayo LEGACY yako na tume itaendelea kuwepo. Usikubali mawazo ya kipuuzi ya kupinga mambo mazuri na mani ya wananchi wenyewe bila shinikizo la vyamya vya siasa.

Tunaamini wajumbe wote ni wajumbe wa MUNGU mwenyewemaana kama mtapoteza fursa ya kujiwekea LEGACY njema, mtawaachia wajukuu zenu sifa mbaya. HONGERENI SANA TUME YA WARYOBA.
 
Back
Top Bottom