Jaji Warioba: Hofu na uoga sababu ya vyombo vya Habari kutoandika matatizo ya Wananchi

Jaji Warioba: Hofu na uoga sababu ya vyombo vya Habari kutoandika matatizo ya Wananchi

The Supreme Conqueror

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2017
Posts
458
Reaction score
1,280
Uwepo wa hofu na uoga umetajwa kuwa sababu ya vyombo vya habari nchini kushindwa kutekeleza majukumu yake na hivyo kugeuka vyombo vya habari vya propaganda na kuishia kuwasifu viongozi.

Waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba ameeleza hayo kwenye uzinduzi wa Ripoti ya Hali ya Vyombo vya Habari na kueleza kwa sasa wananchi wamesahaulika na viongozi kupewa nafasi kubwa kwenye vyombo hivyo.

Yapi maoni yako kufuatia kauli hiyo ya Jaji Warioba kuhusu wananchi kusahaulika, na nini kifanyike kubadili hali hiyo kwenye vyombo vya habari?

Mawazo huru kwa Maendeleo ya Taifa letu.
 
Sasa wao wenye uwezo na nafasi ya kuongea kwa uwazi pasipo kujificha hawafanyi..
Nani afanye?!
 
Vyombo vyenyewe vya habari ni vp? Tangu ulimwengu wa smartphone uanze sikumbuki lini nilinunua gazeti.
Sanasana naangalia taarifa ya habari saa mbili usiku ambayo 90% taarifa zao tayari tushazijua na kuzijadili. Ni swala la muda tu. Magazeti watakuja kushindwa hii biashara.
 
Uwepo wa hofu na uoga umetajwa kuwa sababu ya vyombo vya habari nchini kushindwa kutekeleza majukumu yake na hivyo kugeuka vyombo vya habari vya propaganda na kuishia kuwasifu viongozi...
Hii Mizee ni mijitu ya hovyo inaona CCM inavyoharibu Nchi halafu kwenye mikutano ya chama unaikuta pale mbele. Hawana moral authority ya kuongelea mabaya ya CCM wakati wao ni sehemu ya tatizo.
 
chombo cha ahabaria angalau naweza kuchungulia habari yao angalau kwa asilimia 5% tu ni Azam.ITV na STAR TV hamnaga kitu kabisa siku hizi.wanaishia kuandika habari za tasaf na utumbo mwingine.
 
Back
Top Bottom