makoye2009
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,638
- 1,218
Juzi jaji Warioba alitoa yake ya moyoni wakti akiongea na Baraza la Wanawake huko Bagamoyo. Jaji Warioba ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Mpya alisema vyama vya siasa vimeamua kuingilia uhuru na maoni ya Watanzania kuhusu upatikanaji wa Katiba mpya.
Jaji Warioba aliweka wazi kuwa tume yake haiko tayari kuanzan kupokea maoni mapya yanayopingana na Rasmi ya katiba kama ilivyopendekezwa na Watanzania wengi. Alisema vyama lazima viheshimu maoni na mawazo ya Watanzania na viache kupenyeza mambo ambayo ni ITIKADI za vyama!
Tangu Rasimu ya Katiba mpya itolewe na Tume chama Twawala CCM kimeonekana kutofurahishwa na Rasimu hiyo hasa kwenye kipengele cha Muungano. Katika Rasimu hiyo maoni ya watu wengi walitaka Serikali 3 lakini kwa mtazamo wa CCM wao wanataka serikali 2 ambazo ndizo ziko kwenye mfumo uliopo sasa. CCM waliamua kuitisha vikao vya ndani na kuweka msimamo wao kuwa hili la serikali 3 watalipinga kwa Nguvu zote kwa kuandaa waraka kwenda kwenye mabaraza yote ya Wananchama wa CCM ili waunge mkono seikali 2.
Kila wajumbe wa Tume ya katiba walipokwenda walikutana na maoni yanayofanana sentensi kwa sentensi na nukta kwa nukta yaliyokuwa yakisomwa mbele zao na Wanachama wa CCM waliokuwa wameandaliwa kuwasilisha maoni hayo ya CCM! Kulingana sheria za Tume CCM wameonekana kukiuka sheria na taratibu zilizowekwa. CCM wanaonekana kutaka kulazimisha mambo ili kupata Katiba Mpya itakayokidhi Itikadi zao na si Matakwa ya Watanzania! Hii ni aibu kwa CCM na viongozi wao wote.
Mimi namaliza kwa kusema hivi. CCM wanatakiwa kusoma alama za nyakati na kuelewa nchi iko wapi na inaelekea wapi. Pengine niwakumbushe tu kilichotokea wakti wa Mwalimu JK nyerere(Baba wa Taifa-RIP) katika kura ya maoni kuhusu Tanzania kuwa na Mfumo wa Siasa ya vyama Vingi au kuendelea na mfumo wa Chama kimoja. Baada ya kura ya maoni kuhusu ni mfumo upi Tanzania ifuate ilionekana kwamba 80% walitaka kuendelea na mfumo wa Chama kimoja na 20% walitaka kuwa na mfumo wa Vyama vingi.
Kwa vile Baba wa Taifa alikuwa na AKILI KUBWA iliyokuwa ikiongoza akili ndogo alisoma alama za nyakati na akafikia uamuzi wa kuheshimu maoni ya Wachache ya kuwa na mfumo wa Vyama vingi ambayo ni Demokrasia sahihi na chanya hata kama waliotaka hivyo walikuwa ni wachache! Nawashauri CCM waige mfano wa Baba wa Taifa na waache tabia ya u-kinganganizi kwa mambo ambayo watu hawayahitaji tena hata kama ni wachache. Muungano wa serikali 2 umeonekana una mapungufu mengi kwa muda mrefu sasa na hauna tija! CCM wasitake kuwarudisha Watanzania kwenye ujima!
Tatizo la CCM ni kwamba kwa sasa chama hiki hakina hata mtu mmoja mwenye akili kubwa kama alivyokuwa Mwalimu JK Nyerere. Chama kimejaa watu wenye akili ndogo na dhaifu kifikra,kivitendo hata kimaamuzi. Tusitegemee lolote kutoka CCM kwa uongozi huu wa akina Mwigulu Nchemba,Nnepi Nauye, Kinana,Pinda, Wassira,Mangula na wachovu wengineo ndani ya CCM!
Nawasilisha.