William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,400
..anapelekwa Ubalozini Baada Ya Kupibwa Chini Unaibu Katibu Mkuu Wa Chama ..baada Ya Kuhusika Na Kashfa Ya Ufujaji Pesa Makao Makuu ...pesa Za Uchaguzi Mkuu Ccm..na Pia Pesa Za Kununua Wapinzani..ambapo Kina Akwilombe Walikuwa Wakisainishwa Milioni 2..halafu Anaongezea Sifuri Anasema Amewanunua Milioni 20...mchezo Wake Yeye Na Komba.....pamoja Na Kuwa Ni Kosa Lazima Wamkumbuke ...kwa Kuwa Wote Yeye Na Mwenyekiti Wake Na Sekretariati Lengo Lao Lilikuwa Wizi..yeye Kaiba Pesa..na Chama Kinarubuni Wapinzani!!!..ngoma Droo...mpeni Ubalozi...
Sasa Tunasubiri Kazi Jk Aliyomuahidi Aggrey Mwamry....
hivi mbowe anazo qualification za kuwa rais wetu?
maana ana diploma tu na hana experience ya uongozi
Nimekuwa ninafuatilia postings za Kubwajinga katika threads mbili sasa hii na ile ya Wanajeshi wetu kupelekwa Comoro.
Kimsingi inaonesha kuwa Kubwajinga unakuwa ni mzito wa kuelewa (hata pale unapoelewesha) au hufahamu ni situation gani iliyopo sasa hivi inayompa madaraka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuteua wasaidizi wake mbalimbali.
Kwanza kabisa ni vyema ukaelewa kuwa kazi ya uwakilishi kama ya ubalozi inahitaji mtu mwenye uwezo wa kuongoza, si kila mtaalam ni ana uwezo wa kuongoza. Sifa za uongozi Jaka Mwambi anazo.
Pili, Majukumu ya Ofisi za kibalozi huweza kutofautiana toka nchi moja hadi nyingine kutokana na sababu mbalimbali kama za kiuchumi, kisiasa, kihistoria, kiusalama nk. Kwahiyo Rais huweza kuamteua mtu yeyote mwenye uwezo kuongoza / kuiwakilisha Tanzania. Uwezo huo Rais amepewa kikatiba na ni halali.
Tatu, Ofisi za kibalozi huwa na technical staff ambao ndiyo msingi wa kazi za kila siku za ubalozini. Hawa technical staff ndiyo wataalam unaowasema wewe.
Mwisho kabisa, nikisoma postings zako between the lines zinaonesha udhaifu mkubwa sana, kwani unamwongelea JK kama JK, na siyo JK kama Rais. Ninasema hivi kwa sababu huonyeshi ni wapi Rais amekiuka taratibu za ki-madaraka na ki-mamlaka katika kufanya uteuzi wa Jaka Mwambi.
Inawezekana unamchukia JK kwa sababu ambazo unazifahamu wewe mwenyewe kwahiyo unatumia muda na fursa iliyopo hapa JF kuandika na kutoa 'nyongo', any way kama ni therapy kwako basi mwandikie barua then ipeleke Ikulu.
Mkuu Punda,
Nashukuru kuwa umevutiwa na postings zangu ingawa unatengeneza makunyansi contents zake. Hii inaonyesha ubora wake hata kwa wliopotoka, otherwise usingetumia muda wako kusoma na hata ku-comment. Shukhran.
Kuelewa kuna aina nyingi. Mbili za kidemokrasia ni 'your way' or 'my way' lakini sio 'the highway'. Yule anayekuwa upande wa majority ndio anayetambulika kuwa mshindi, upande ambao always nimeangukia. Kwa hiyo, conclusion yako ya kusema KJ haeleweshweki, meanining sifuati unachotaka wewe, haina uzito. Let's have constructive discussion sio kukaa bweteka tu na kuwapigia makofi walioko madarakani kwa vile tu labda tunanufaika na huo uzembe wao. Jenga hoja, kama iko sawa hata mimi nitaku-support.
Mkuu, tupatie hizo sifa za Jaka za kumzidi Chokala, maana mara ya mwisho nakumbuka uongozi chamani alionekana hafai.
Hii inakubalika kuwa ofisi za kibalozi zinatofautiana. Ndio maana tunahitaji wasifu wa Jaka wa sasa unaomfanya afae kutuwakilisaha Russia. Tulio nao sisi ni ule wa yeye kushindwa kazi Tanga, Iringa, CCM HQ n.k.
Kama wataalamu wapo yeye anafuata nini kuongeza gharama na carbon footprint?
Unfotunately humu mtandaoni, JK ni JK kama binadamu raisi wa nchi na sio mungu kama kama ilivyo kwako. Hapa tunaongea vile roho inapenda.
Simchukii JK kwani ni dhambi nami ni muumini wa dhati, lakini ninachukia sana sana sanaaaa yale yeye, wanamtandao na wapiga debe wao wanayoitendea nchi yangu. Sijui wewe mwenzetu unayafurahia? Hebu tufahamishe.
Kwa kawaida Mwalimu hufundisha na baadae hutoa jaribio kuangalia wanafunzi wameelewa kwa kiasi gani, lakini bado kuna wengine hupata ZERO.
Kwaheri!!!!
1. Chokala, amemaliza muda wake ndio maana Mwambi anaenda kumbadili hivi hili nalo linahitaji debate?
2. Nafasi ya mwisho ya Mwambi, nationally, ilikuwa ni kama ya Mh. Zitto, kule Chadema, yaaani naibu katibu mkuu wa chama tawala, nafasi ambayo mara ya mwisho ilishikwa na waziri mdogo wa nje Ndugu Idd
3. Mkuu labda utuweke sawa, kwa maoni yako bongo kiongozi wa taifa anayefaa kwa standards zako ni yupi?
Hoja ya kwamba wataalam wapo na asipelekwe Mwambi ni hoja dhaifu mno, ni sawasawa na kusema Sir Alex Furguson au Arsene Wenger sio muhimu na hawahitajiki katika timu zao kwani wachezaji wenye vipaji wapo (Ninajaribu kutoa mifano rahisi kabisa ili KJ aelewe)
FMES,
..Seifu Iddi alikuwa Foreign Service Officer his whole career. Alipanda ngazi mpaka kuwa Balozi wetu China. Baada ya hapo akateuliwa Naibu Katibu Mkuu CCM, na sasa ndiyo amerudi Mambo ya Nje kama Naibu Waziri.
..Najua hayo yote unayafahamu, sasa sijui kwanini unajaribu kumlinganisha Balozi.Seif Iddi na Capt.Jaka Mwambi.
..Raisi ana mamlaka ya kuchagua Mtanzania yeyote yule kuwa Balozi. Sasa hiyo haihalalishi Raisi ateue hata Watanzania wenye MINIMUM QUALIFICATIONS kutumikia ktk nafasi hizo.
..Tanzania ni nchi masikini. Tunapaswa kutumia RASILIMALI zetu, ikiwa ni pamoja na WATAALAMU, kwa umakini mkubwa. Tunapaswa kufanya maamuzi yetu kwa umakini mkubwa kuliko mataifa tajiri na yaliyoendelea.
..Nilitarajia Raisi ambaye ame-serve miaka 10 kama Waziri wa Mambo ya Nje, angeteua Mabalozi from the cream-of-the cream ya Wataalamu wetu wa Diplomasia na Mashirikiano ya Kimataifa. Huu uteuzi wa Capt.Jaka Mwambi unatia mashaka kwa kila anayefuatilia utendaji na ufanisi wa Balozi zetu.
..Wataalamu tunao, kwanini hatuwapi nafasi kutumikia? Kwanini Balozi zetu ziendelee kuwa vichaka vya kuficha vigogo walioshindwa ktk majukumu yao ya awali? Adadi Rajabu alishindwa kama Dir' wa CID, Lt.Gen.Mayunga alituhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za CCM Kilimanjaro, na wengine wengi sina haja ya kuwataja hapa.
Seifu Iddi alikuwa Foreign Service Officer his whole career. Alipanda ngazi mpaka kuwa Balozi wetu China. Baada ya hapo akateuliwa Naibu Katibu Mkuu CCM, na sasa ndiyo amerudi Mambo ya Nje kama Naibu Waziri.
]..Najua hayo yote unayafahamu, sasa sijui kwanini unajaribu kumlinganisha Balozi.Seif Iddi na Capt.Jaka Mwambi.[/B
..Raisi ana mamlaka ya kuchagua Mtanzania yeyote yule kuwa Balozi. Sasa hiyo haihalalishi Raisi ateue hata Watanzania wenye MINIMUM QUALIFICATIONS kutumikia ktk nafasi hizo.