Jakaya Kikwete apongeza juhudi za Kuhamia Dodoma

Jakaya Kikwete apongeza juhudi za Kuhamia Dodoma

The Supreme Conqueror

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2017
Posts
458
Reaction score
1,280
1684640715371.jpg

Rais Mstaafu wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete kwa niaba ya Wastaafu amemshukuru Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaalika kushuhudia uzinduzi wa Ikulu mpya ya Chamwino Dodoma huku akisema leo historia leo historia mpya imeandikwa Tanzania “Historia imeandikwa tena imeandikwa kwa wino wa dhahabu”

Akiongea Ikulu Dodoma Dkt. Kikwete amesema “Hili ni jengo ambalo tumejenga wenyewe, Wataalamu wetu walichora wakasanifu, tumetoa pesa zetu wenyewe kujengwa na leo limekamilika”

“Tukio hili linahitimisha dhamira ya Baba wa Taifa ya kuhamishia Makao Makuu ya Dar es salaam kuyaleta Dodoma, uamuzi ulifanyika mwaka 1971 lakini leo Mama yetu Rais Samia umekamilisha maana kilele cha uamuzi ule ni Rais kuhamia Dodoma na kuwa na Ofisi yakeDodoma”

“Katika kila awamu kuna yaliyofanyika, maana Uongozi ni kazi ya kupokezana vijiti unafanya anakuja mwenzako anafanya mpaka mnafika mwisho wa safari, yapo yaliyofanywa na Mwl Nyerere, akaja Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na katika kipindi changu niliamua tujenge Chuo Kikuu kikubwa zaidi Dodoma pale Chimwaga, nikaelekeza Ofisi ya Rais na Makazi ya Rais yajengwe Chamwino na Ofisi za Mawaziri zijengwe karibu na hapo, kukawa na mjadala nikawaambia nendeni Malyasia mkajifunze walivyojenga unavuka Makazi ya Mawari mbele ndio kuna Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa”

“Mh. Rais wa awamu ya tano Dr. Magufuli akaanza ujenzi na Rais Dkt. Samia kazi ile umeikamilisha na umeikamalisha kwa kiwango cha juu sana, nakupongeza sana Rais kwa Uongozi wako na nawapongeza wote walioshiriki ujenzi, Mh. Rais unafanya mambo mazuri katika Nchi yetu mwenye macho haambiwi tazama, mwenye masikio haambiwi sikia, umepokea miradi mikubwa ungeweza kusema unaanza ya kwako lakini umesema kila kilichoanzishwa na Mtangulizi wako unakikamilisha”
 
Back
Top Bottom