MwanaDiwani
JF-Expert Member
- Mar 22, 2013
- 5,536
- 2,266
MWENYEKITI wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete amesema ili nchi iwe na umoja, kuna umuhimu wa mchakato wa kutoa maoni ya kuandikwa kwa Katiba mpya, ufanyike kwa umakini.
Alisema hayo mjini hapa jana, wakati akifungua kikao cha cha Baraza la Katiba la CCM ngazi ya Taifa, ambapo kikao hicho kinahudhuriwa na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC).
Kama tutaingiza takataka katika kutoa maoni, tutavuna takataka katika kupata Katiba mpya, alisema Rais Kikwete katika hotuba yake hiyo.
Rais Kikwete alisema iwapo wajumbe wa NEC, watafanya kazi hiyo kwa umakini mkubwa, nchi itaendelea kuwa katika hali ya utulivu na mshikamano.
Alisema kama kazi hiyo itafanyika vizuri, kutakuwa na nchi yenye utulivu; na ikifanyika vibaya, kwa kuingiza takataka, hata matokeo yake yatakuwa ni takataka.
Ni lazima kuhakikisha kazi hii, inafanyika kwa utulivu ili nchi iendelee kuwa na umoja, alisema. Alisema anapenda kuona kila mmoja, anatoa hoja na kuacha kupiga kelele; na hata wale wanaokosoana, wafanye hivyo taratibu. Kila mmoja atoe hoja, aache kupiga kelele, mkosoane kwa utaratibu, mjumbe usiibue usichokitaka, eleza kile unachokitaka na ukijengee hoja, alisema.
Alisema wengine walikuwa ni wajumbe kwenye mabaraza yaliyopita na sasa wapo; na kutaka watoe miongozo; na kila mmoja asione haya, kutoa yale anayofikiria yatasaidia.
Nasisitiza tuvumiliane, wengine wanaweza kuwa na mawazo tofauti. Kwani mtu akitoa mawazo yake, usiyoyapenda, usipige kelele kwa kuwa tusipokuwa makini, hatutakuwa tunajadili Katiba, bali tutakuwa tunapiga kelele, alisema Rais Kikwete.
Pia, alisema vyama vya siasa vimepata fursa kama taasisi, vitoe maoni ya rasimu ya katiba; na kazi inayofanya na NEC ni kutengeneza utaratibu mzuri wa namna ya kuingiza mawazo ya wanachama wa CCM kwenye rasimu ya Katiba.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa taarifa yake, alisema kuna jumla ya mabaraza ya Katiba 18,879 ya CCM, ambapo wanachama milioni 2.6 walishiriki kutoa maoni hayo kupitia mabaraza hayo.
Alisema bado maoni kutoka Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT), ambapo yanaendelea kukusanywa na yanatarajiwa kufikishwa katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba, mara kazi hiyo itakapokamilika.
Sakata la Bukoba
Wakati Rais Kikwete akionya juu ya umakini katika Katiba mpya, Kamati Kuu ya CCM imewaita Dodoma viongozi wa chama hicho mkoani Kagera, akiwemo Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii na Meya wa Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani kwa ajili ya mahojiano.
Hatua hiyo inafuatiwa na sakata la kuvuliwa uanachama madiwani wanane wa Manispaa ya Bukoba. Katika mkutano wake na waandishi wa habari jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema viongozi sita wameitwa kwa ajili ya mahojiano hayo mjini Dodoma.
Licha ya viongozi hao kuitwa, Nnauye alisema hatma ya Mwakilishi wa Kiembe Samaki kupitia CCM, Mansour Himid Yusuf ipo mikononi mwa NEC iliyokaa kuanzia jana.
Alitaja walioitwa mjini Dodoma kwa ajili ya mahojiano kuwa ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera, Katibu wa CCM Mkoa, Katibu wa CCM Wilaya ya Bukoba Mjini, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukoba na Meya wa Manispaa ya Bukoba.
Alisema viongozi hao, walitarajiwa kufika mjini Dodoma jana ili kuweza kuonana na Kamati Kuu kwa ajili ya mahojiano zaidi. Nnauye alisema Kamati Kuu baada ya kushughulikia sakata la Madiwani wa Bukoba, limeamua kuwaita Dodoma viongozi hao na wanatakiwa kufika Dodoma kuonana na Kamati Kuu leo kwa ajili ya mahojiano.
Hata hivyo, alisema baadhi ya viongozi hao, wakiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera wapo Mjini Dodoma, wakiendelea na kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM. Baada ya mahojiano na viongozi hao Kamati Kuu itatoa taarifa ya hatua zaidi dhidi ya sakata hilo la madiwani, alisema.
Sakata la kuvuliwa madaraka kwa madiwani wanane wa CCM wa Manispaa ya Bukoba ilileta sintofahamu kutokana na CCM taifa kupinga kitendo hicho.
Madiwani hao wanatajwa kuwa ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukoba, Yusuph Ngaiza ambaye ni Diwani wa Kata ya Kashai, Diwani wa kata ya Kitendagulo, Samwel Ruangisa, Diwani wa Viti Maalum Murungi Kichwabuta, Diwani wa kata ya Nyanga, Deusdedith Mutakyawa na Diwani wa kata ya Miembeni, Richard Gaspar ambaye pia ni Naibu Meya.
Wengine ni Diwani wa kata ya Buhemba, Alexander Ngalinda, Diwani wa kata ya Hamugembe, Robert Katunzi pamoja na Diwani wa Kata ya Ijunganyondo, Dauda Kalumuna.
Kuvuliwa udiwani kwa viongozi hao, kulipingwa, kutokana na waliofanya hivyo walikiuka kanuni na taratibu za Katiba. Kutokana na hali hiyo, Nnauye aliwataka madiwani hao kuendelea na kazi hadi hatua zaidi, zitakapochukuliwa na Kamati Kuu itakapokutana.
Mvutano huo wa kisiasa, baina ya Kagasheki na Amani unadaiwa kutishia kukigawa chama hicho mkoani Kagera, hali iliyofanya CCM ngazi ya taifa kuingilia kati suala hilo.
[video=youtube_share;G6_PyJm4IIE]http://youtu.be/G6_PyJm4IIE[/video]
Chanzo: Habarileo.