Jalada la Kesi ya Jaji Rugazia latupwa kwa DPP

Jalada la Kesi ya Jaji Rugazia latupwa kwa DPP

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
KUTOKANA na wadhifa aliokuwa nao mtuhumiwa wa kesi ya usalama barabarani ya kukabiliwa na shtaka la kuua inayomkabili Jaji wa Mhakama Kuu ya Tanzania, Protest Rugazia [56] jalaada linalohusiana na shtaka hilo limepelekwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Masht Hatua hiyo imechukuliwa na Polisi Kanda Maalum ya Dar es alaam ili kuzingatia taratibu mbalimbali na sheria na uandaaji wa kuongoza shauri hilo.

Kamanda wa Kova, aliwaeleza wanahabari kuwa, jeshi hilo lilishafatilia mwenendod wa ajali hiyo na tarawtibu za kiupelelzi zimeshakamilisha na kutokana na mshitakwia katika shauri hilo kuwa na wadhiwa inatakiwa tuongozwe taratibu za mashitaka na DPP.

Katika kesi hiyo, Jaji Rugazia anakabiliwa na shitaka la kusababisha kifo cha mtembea kwa miguu, aliyetambulika kwa jina la Salehe Omary, mkazi wa Msasani, Dar es Salaam katika barabara ya Bagamoyo, Oktoba 3 mwaka huu.

Na aliweza kujeruhi watu wengine watatu waliotambulika kama Nasibu Hassan[28] mkazi wa Kitunda, Rahma mwanafunzi wa chuo cha IFM na Issa Idd [30] mkazi wa Kinondoni
 
Hivi "Judicial immunity" haifanyi kazi kwenye jambo hili?
 
Hivi "Judicial immunity" haifanyi kazi kwenye jambo hili?

Judicial immunity ipo kwenye maamuzi yanayofanywa na hakimu au jaji akiwa mahakamani na akisikiliza na kuamua kesi au mashauri lakini hakuna mwanya huo kwa matendo nje ya uendeshaji wa kesi mahakamani-Ufafanuzi tu huo.
 
Majaji si wanatakiwa wanaendeshwa wakati wote kuwaepusha na issue kama kama haya?
Siku tutasikia Pinda au Kikwete kagonga naye
 
Back
Top Bottom