Jamaa aelezea safari yake ya biashara miaka 13 kwa picha nne

maskini ana connection gani?
tusiweke visingizio, kutoboa bila connection inawezekana
Ili ufanikiwe unahitajika kufanya kitu sahihi na sehemu sahihi, na hapo inahtajika taarifa sahihi kutoka kwa watu sahihi.....hii itakufanya ukosee mara chache na ufike haraka unapopataka..other factors should remain costant eg, Juhudi, Bidii, uvumilivu, Ujuzi, ubunifu n.k.....najua hukunielewa
 
Huyo jamaa sio mtu wa kukata tamaa, na aliamua kuchagua kusimamia jambo moja tu, biashara ya nguo.

Tokea 2005 hadi 2018, amejikita kwenye eneo hilo hilo na amefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana. Wengi tunashindwa kupata matokeo chanya kwa kujaribu kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja.

Hata hivyo picha hazionyeshi wala kuelezea changamoto alizopitia, nnachotaka kusema kila penye mafanikio kuna changamoto zake, kupambana nazo na kuzitatua ndio kutakutofautisha na wengine.
 
yes hata yeye anamtegemea sana huyo anayetembea na bahasha kutafuta take home ya 400K
Tatizo lako unataka kuaminisha ametusua kwa kusaidiwa,je wewe huko kwenye kibarua chako hakuna wa kukusaidia?Hapo cha kujifunza kwa Huyo jamaa ni kua alianza na alichokuwa nacho+uaminifu+malengo.Sasa hata akiwa anapewa malikauli inatokana na kukubalika kwake na wafanyabiashara wakubwa.Nilichojifunza tuache kudharau kazi,sio kujiita mchumi wakati huwezi kulibadilisha hilo jina kuwa pesa+ajira.
 
kutoka hatua ya kwanza mwaka 2005 kwenda hatua ya pili mwaka 2009 lazima kuna mtu alimshika mkono kwa kumuongezea mtaji


Mkuu sikupingi lakini jaribu kutambua na kuthamini juhudi za huyu jamaa kwanza.

Unakubali kwamba sio kila anaeshikwa mkono anafanikiwa?
Watu wangapi wamepewa kila kitu na wameishia kuleta fedheha?

Iwe itakavyokua, upambanaji wa jamaa umechangia kwa kiasi kikubwa sana kumfikisha hapo.
 
Bila connection hapa duniani huwez kutoboa...huwez jua wakat anaanza ni watu gan wa muhimu katika kupata taarifa walikuwa wamemzunguka...amekomaa na ameweza bigup

Hili neno connection, linatumika na vijana wengi sana kama mwamvuli wa kushindwa kwao... hyo unayoiita connection ni matunda ya mapigano ya mda mrefu...
Tafadhali... tupa huo mwamvuli, uanze kupambana.
 
Hili neno connection, linatumika na vijana wengi sana kama mwamvuli wa kushindwa kwao... hyo unayoiita connection ni matunda ya mapigano ya mda mrefu...
Tafadhali... tupa huo mwamvuli, uanze kupambana.
Hujui unachokiongea...utaendelea kubaki hapo hapo ulipo
 
Hilo ni janga la taifa.
Siku zote nasema tatizo sio unapata kiasi gani, unafanya nini na unachokipata ndio msingi wa kufanikiwa kwako.

Ni kweli kabisa
Ndiyo maana wapo wenye mishahara ya daraja la chini lakini wanafanya maendeleo na wapo wenye kipato cha kati wanaishi kwa mikopo

Kusimamia kitu kimoja kunafanya kuwa mzoefu kwenye hilo eneo
Utazijua changamoto zake,matatizo na hata opportunities za hilo eneo
Wengi tunafanya hichi tunaacha ukiteleza kidogo unahama kabisa
 

Wanaobisha hawajaexperience

Hata upewe million Mia,uwe na connection Tanzania nzima kama huna mission,Vision na nidhamu ya pesa utabaki hapo hapo
 
kwa hiyo kwa akili yako unataka kusema mwaka 2005 alipo kuwa machinga,amaefanya umachinga ndani ya miaka 3 awe na duka hapo juu kwenye picha namba 2?
Sio mitatu ya umachinga ni 4 au 5 kabisa. Kwa kujibana na kupiga kazi inawezekana.
 
maskini ana connection gani?
tusiweke visingizio, kutoboa bila connection inawezekana
Watu ndio mafanikio...! Peke yako huwezi kufika popote ila na wewe uwe na juhudi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…